Header Ads

Responsive Ads Here

SHABIKI MKUBWA WA TIMU YA YANGA MAARUFU KWA JINA LA ALLY YANGA AFA AJALINI HUKO MPWAPWA MKOANI DODOMA


index
MWANACHANA wa klabu ya Yanga na mpenzi maarufu wa soka nchini, Ally Mohamed anayejulikana zaidi kwa jina la utani ‘Ally Yanga’ amefariki dunia leo baada ya ajali ya gari iliyotokea, eneo la Mpwapwa, Dodoma.Taarifa zinasema Ally Yanga alikuwa kwenye msafara wa mbio za Mwenge kabla ya kupata ajali hiyo barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipogoro na kufariki hapo hapo.
Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam
Aliibukia Ubungo miaka ya nyuma kidogo ambako alikuwa anafanya shughuli ya kusajili laini za simu za mkononi katika vibanda vilivyokuwa pembeni ya kituo kikuu cha mabasi ya mikoani, Ubungo Terminal.
Na alianza kuonekana Uwanja wa Taifa pamoja na kikundi cha mashabiki wa Yanga cha Ubungo Terminal, ambako ndipo lilipokuwa tawi lake.
Ally Yanga enzi za uhai wake akiishabiki Yanga Uwanja wa Taifa katika mechi tofauti
Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.

No comments