Header Ads

Responsive Ads Here

Serikali Yatambua Jitihada Za TBL Group Katika Utunzaji wa Mazingira


unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani  kwa niaba ya kampuni, Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Afisa mtendaji wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin katika hafla maalum iliyofanyika nyumbani mwa Makamu wa Rais mwishoni mwa wiki (Katikati) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya  Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh.January Makamba

1
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Afisa mtendaji wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin akishiriki pamoja na wageni wengine waalikwa katika Iftar iliyoandaliwa na Makamu wa Rais,Mh. Samia Suluhu Hassan
…………………….
-Yatunukiwa cheti cha shukrani kwa kufanikisha na kushiriki Siku ya Mazingira Duniani
Kampuni ya TBL Group imepewa cheti cha shukrani kutokana na jitihada ambazo imekuwa ikizifanya kutunza mazingira ikiwemo kushiriki kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika kijijini Butiama mkoani Mara mwanzoni mwa mwezi huu.
Cheti cha kutambua juhudi hizo kimetolewa na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan, katika hafla maalumu iliyofanyika mwishoni mwa wiki na kilipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Afisa mtendaji wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin.
 Katika maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani 2017 Kampuni ya TBL Group iliyopo chini ya kampuni ya kimataifa ya vinywaji ya ABInBev ilitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya siku ya mazingira duniani nchini ya “Hifadhi mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya Viwanda, ambapo wafanyakazi wake walishiriki katika shughuli za usafishaji mazingira na upandaji miti.
Mazingira ni suala ambalo kampuni  imekuwa inalipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa katika moja ya malengo ya kampuni mama ya TBL Group ya ABInBEV inayojulikana kama ‘Kujenga Mazingira ya Kuishi katika Dunia iliyo safi’ suala la utunzaji mazingira linatekelezwa kwa vitendo katika maeneo yote  ya biashara za kampuni.
 kwa kufuata mwongozo huu kampuni imejiwekea malengo ya kufanikisha kuhusiana na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya matumizi mazuri ya maji katika mchakato wa uzalishaji, kutumia nishati mbadala zisizochafua hewa, kushiriki kampeni za kupanda miti na utunzaji wa vyanzo vya maji,kutumia vifungashio rafiki kwa mazingira.
Kuhusiana na matumizi ya maji kwa umakini  TBL imepunguza matumizi ya maji katika mchakato wa uzalishaji wa bia  kutoka hectolita 6 za maji zilizokua zinatumika katika miaka ya karibuni hadi hectolita 3.6 kwa kila lita moja ya bia inayozalishwa kwa sasa na inaendeleza mkakati wa kupunguza matumizi zaidi ambapo pia imekuwa ikifanya utakatishaji wa maji taka  na kuharibu taka ngumu na nyepesi kwa kutumia teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki kwa mazingira.
Pia kampuni tayari imeanza kutekeleza hatua za kufanya uzalishaji kwa kutumia nishati mbadala zisizokuwa na athari kwa uchaguzi wa hewa ambapo katika kiwanda cha TBL Mwanza kinafanya uzalishaji kwa kutumia mashine zinazozalisha nishati zinazotokana na pumba za mpunga na katika kiwanda cha TBL Mbeya zimefungwa paneli za umeme wa jua ambayo inawezesha kupatikana umeme wa jua unaotumika katika baadhi ya shughuli za mchakato wa uzalishaji.
 TBL Group inaliangalia suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji sio kwa kiwango cha maslahi ya viwanda vyake kupata malighafi tu bali kwa jamii nzima ambapo kampuni inafanyia biashara  kwa kuwa sera ya kujenga ‘Dunia Maridhawa’ (Better World) inashahabiana  Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa  (SDGs)  na suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ni moja ya suala ambalo limepewa umuhimu mkubwa.
Kupitia sera ya kampuni ya ‘Kujenga Dunia Maridhawa’kampuni imeweza  kutekeleza kwa vitendo kanuni za utunzaji wa mazingira, Kuhamasisha jamii unywaji wa kistaarabu na kuunga mkono jitihada za serikali kusaidia kufanikisha changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii hususani katika sekta ya afya,usalama barabarani na elimu na siku zote kampuni na wafanyakazi wote tutaendelea kufanikisha  uwekezaji wenye kuleta manufaa kwa jamii nzima.
Sera ya kujenga Dunia Maridhawa ya ABInBev ambayo inatekelezwa katika maeneo yake yote ya biashara imejikita katika ufanikishaji wa malengo makuu matatu ambayo ni ‘Dunia inayokua ‘ inayolenga kukuza shughuli mbalimbali na kuwapatia watu fursa ya kujiendeleza kimaisha,’Kujenga Dunia iliyo safi inayolenga kulinda mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo na ‘Kujenga Dunia ya watu wenye Afya ambayo inahimiza  utumiaji wa vinywaji kistaarabu bila kuleta athari kwa jamii.

No comments