Header Ads

Responsive Ads Here

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI KUHUSIANA NA KIFO CHA MAREHEMU , MZEE KHAMIS MKADARA.

index

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimepokea kwa mshituko  na  masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mjumbe  wa Baraza la Wazee wa CCM Pemba,  Marehemu Mzee Khamis Mkadara aliyefariki Juni 7, 2017 baada ya kusumbuliwa muda mrefu na Maradhi ya kawaida na kuzikwa Kijijini kwao Wawi Mkoa wa Kusini     Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi” kwa niaba ya Viongozi, Watumishi na Wanachama wote wa CCM, ametuma salamu za rambirambi kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Mzee Mkadara na kuwaomba kuwa na moyo wa subra katika wakati huu mgumu wa maombolezi ya msiba huo.  Bila ya shaka kifo cha marehemu kimeacha pengo kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi na Taifa letu kwa ujumla.

Dkt. Mabodi amesema  Chama Cha Mapinduzi kimempoteza mwanachama mahiri, mchapakazi, hodari na mpenda watu wa rika na jinsia zote na kwamba kifo chake kimekuja wakati Chama bado kinamuhitaji  kutokana na utumishi wake uliotukuka.
Marehemu Mzee Mkadara alizaliwa Mwaka 1927 na kuanza elimu ya Quran katika Madrasa mbali mbali za Wilaya ya Chake chake ambapo baadaye katika ujana wake akajishughulisha na masua la ya Kisiasa katika dhana nzima ya kudai Uhuru wa Visiwa vya Zanzibar.
Mzee Mkadara kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa  Chama cha Shirazy Association na baadae kikaungana na Chama cha African Assocition na kuzaliwa kwa chama cha Afro Shirazy Party pia  Katika Utumishi wa Chama aliwahi kuwa Mwenyekiti wa ASP wa Wilaya ya Chake chake mwaka 1973 na baada  ya  kuzaliwa Chama cha Mapinduzi mwaka 1977 aliendelea na wadhifa huo hadi mwaka 1997, ambapo hadi anafariki alikuwa ni Mjumbe wa Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar kwa upande wa  Pemba.
Mzee Khamis Juma Mkadara  ameacha Kizuka Mmoja, Watoto Wanane na Wajukuu 33
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amin

No comments