Header Ads

Responsive Ads Here

RIDHIWANI APONGEZWA AAMBIWA MTOTO WA NYOKA NI NYOKA


1

RIU1RIU2
Na Mwamvua Mwinyi ,Chalinze
Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,amekemea wanaodhihaki utendaji kazi wa rais .dk.John Magufuli na kudai anakonga nyoyo za wananchi wanyonge kwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili .
Amesema haoni aibu kumuunga mkono rais,na Chalinze inaendelea kutamba kwa hatua mbalimbali za kimaendeleo na kiuchumi zinazochukuliwa .
Aidha Ridhiwani hakusita ,kutoa kilio cha maji licha ya serikali na Chaliwasa kupambana ili kuondoa tatizo hilo kwa wanaChalinze .
Akizungumza katika ziara ya rais dk .Magufuli aliyoifanya Bagamoyo ,mbunge huyo alisema ,anaipongeza serikali na yeye anaendelea kusimamia kero zote ili kuhakikisha Chalinze inapiga hatua na kuwa katika sura mpya .
Alisema hatokuwa nyuma kuiunga mkono katika hatua zinazochukuliwa ikiwemo kupambana na Ufisadi .
“Kama yupo mtu mwenye shaka na utayari wako na uchapakazi wako juu ya sera ya viwanda basi aje Chalinze kuona maendeleo yaliyopo ,na tunatamba kwa hilo.” Tunajua wewe ni kazi tu na sisi hapa chalinze ni kazi tu. “
Ridhiwani alisema ,tatizo la maji bado ni kubwa hivyo ameiomba serikali ione umuhimu wa kushirikiana na wawekezaji wanaojitoa kusaidia changamoto hiyo .
“Alimpongeza Subash Patel na mwekezaji kampuni ya vigae Twyford kilichopo Pingo kwa kuonyesha nia yao kusaidia tatizo la maji ” aliongeza Ridhiwani .
Ridhiwani alibainisha halmashauri yao inaongoza kwa makusanyo ya mapato ya ndani kwa asilimia 102 .
“Mh. Raisi , tumejipanga halmashauri yetu inajiwezesha yenyewe.Zaidi ya Milioni 200 zimepelekwa kuwezesha vikundi vya ujasiriamali katika mikopo ya vijana na wanawake.
Ridhiwani anashirikiana vyema na halmashauri hiyo ,na ameshasaidia ujenzi wa shule ya Moreto iliyowahi kuungua.
Pia alishatoa gari la wagonjwa,vitanda katika shule za msingi na sekondari jimboni hapo ,vitabu vya kujifunzia kwa shule hizo.
Ridhiwani aliwahi kutoa mabati na mifuko ya saruji vilivyogharimu mamilioni ya fedha katika ujenzi wa baadhi ya madarasa ,zahanati ,na ofisi mbalimbali za mashuleni na vijiji .
Nae Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,alikumbushia halmashauri ya Chalinze ,kupewa majengo yaliyokuwa yakitumika na mkandarasi aliyekuwa akijenga barabara ya Msata -Chalinze .
Rais Magufuli aliuambia umati uliokuwepo katika shughuli hiyo kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka.
Alisema ni hakika Ridhiwani anaonyesha uwezo wa kiuongozi na sio kama kachaguliwa kwa mgongo wa mtu .
Dk.Magufuli alimfananisha Riz na Baba yake dk.Kikwete aliyewahi kuwa raisi Wa Jamhuri ya Tanzania wakati wa awamu ya Nne na kusema kweli kaya hiyo ni ya wanasiasa .
Mbali na hayo aliikabidhi halmashauri ya Chalinze majengo ambayo yalitumiwa na Mkandarasi Wa barabara ya Msata wakati wa Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Msata.
Alieleza anatoa majengo hayo bure na halmashauri hiyo itajipangia matumizi yake na kuiomba itunze mali zilizomo kwenye majengo hayo.
WAKATI HUO HUO ,mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Ndikilo alimshukuru rais dk.Magufuli kwa kufanya ziara ya siku tatu Mkoani hapo .
Alieleza ,kwa hakika wananchi wamefarijika kwa mikutano aliyozungumza nao ,kukagua,kutembelea kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi ya kiuchumi na kimaendeleo ikiwa ni sanjali na miundombinu ya barabara,maji na uwekezaji ,kuanzia june 20 hadi June 22 .
Mhandisi Ndikilo ,alielezea kwamba,wananchi walio wengi watakuwa wamejua namna serikali yao inavyofanya kazi kwa manufaa ya Taifa na mkoa .
Kwa upande wa wananchi wa wilaya ya Kibaha na Bagamoyo ,walimshukuru dk.Magufuli kwa kuwatembelea na kufuturu nao pamoja .
Mgeni Msafiri ,alisema hakika wamefarijika na ziara hiyo na wamepokea yale aliyoyasisitiza kwa jamii ikiwemo kusomesha watoto hasa Wa kike kwa manufaa yao baadae .
“Alituhimiza pia kufanya kazi ,kuacha uvivu na kutumia viwanda vilivyojengwa Mkoani kwetu ” alisema Mgeni.
Jesca Mingo ,alisema haijawahi kutokea kwa miaka mingi rais kulala ikulu ndogo ya Mkoa Wa Pwani .

No comments