Header Ads

Responsive Ads Here

RC TABORA ASIMAMISHA MADUKA MAWILI KWA KUUZA BIDHAA ZINAZOHATARISHA AFYA ZA WATUMIANI


unnamed
Na Tiganya Vincent Tabora 9.6.2017

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ameongoza zoezi la ukaguzi wa baadhi ya maduka ya dawa na chakula na hatimaye kufunga mawili baada ya kubainika kuuza chakula katika mazingira machafu na linguine vipodozi na sabuni zilizopigwa marufuku hapa nchini.

Bw. Mwanri kwa kushirikiana na Maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa ametekeleza zoezi hilo la kushitukiza jana kwenye Mtaa wa Ujiji kata ya Gongoni katika Manispaa ya Tabora.

Alisema kuwa yeye na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wana dhamana ya kuhakikisha wakazi wote wa Mkoa huo wanakula chakula ambacho hakihatarishi maisha yao na kutumia vipodozi ambavyo havina kemikali.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa vipodozi vyenye viambata vyenye sumu vilivyokamatwa katika duka la vipodozi vitaorodheshwa ili vijulikane kwa ajili ya kuanda taratibu za kumshitaki mhusika na hatimaye kuteketezwa kabisa.
Aliwaagiza Maafisa wa TFDA kuhakikisha vipodozi na sabani zenye sumu zilizokamtwa hazitoroshwi na kama wataona wanahitaji msaada wa Polisi wamweleze ili bidhaa zote zisizofaa zichukuliwe.

Katika ukaguzi mwingine Mkuu huyo wa Mkoa alilazimika kufungia duka la chakula la mfanyabiashara mmoja kwa kosa la kuweka bidhaa za kula binadamu katika mazingira machafu ambayo yahatarisha maisha ya watumiaji.

Alisema kuwa sehemu ya kuuzia chakula ni sharti iwekwe katika mazingira ambayo ni safi  na salama kwa mtu anayetumia bidhaa hiyo ili kulinda afya yake.

Bw. Mwanri aliongeza kuwa chakula cha binadamu hakiwezi kuwekwa kama vile kinavyowekwa chakula cha kula mifugo na kuongeza kuwa hata mifugo wakati chakula chake uwekwa vizuri.

Kwa upande wa Meneja wa Kanda ya Magharibi wa TFDA Dkt.Edgar Mahundi alisema kuwa bidhaa zilizokamatwa zinatarajiwa kuteketeza mara baada ya wahusika kufikishwa Mahakamani na chombo hicho kutoa uamuzi.
 
Alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha kabla ya kunua bidhaa wanaangalia kama haijaisha muda wa matumizi na pia kama haiku katika orodha ya bidhaa zilizopigwa marufuku.

Meneja huyo wa Kanda alisema kuwa sasa wanatarajia kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara kwa sababu bado wafanyabiashara wanauza hizo zilizopigwa marufuku.

Meneja huyo aliongeza kuwa ni vema wananchi wakasaidia kuwafichua watu wote wenye tabia ya kuuza bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu.
 

No comments