Header Ads

Responsive Ads Here

PEMBA:MWAKILISHI WA JIMBO LA MICHEWENI AMEWATAKA WAJUMBE WA KAMATI ZA SIASA ZA MATAWI KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI

Na  Masanja Mabula –Pemba ….

MWAKILISHIwa Jimbo la Micheweni Shamata Shaame Khamis amewataka wajumbe wa kamati za siasa za Matawi na Wadi katika jimbo hilo kushirikiana na vyombo vya ulinzi kudhibiti matumizi haramu ya bandari bubu zilizomo katika Jimbo hilo .

Amesema katika Jimbo hilo kuna utitiri wa bandari bubu nyingi ambazo zinadaiwa kutumika kupitishia magendo pamoja na wahamiaji haramu , na kwamba kuna hitajika  juhudi za makusudi kuzisimamia ili kusiwepo na matumizi  hasi ya bandari hizo .
Akizungumza  na  wajumbe wa kamati za siasa za Matawi , wadi na Jimbo , katika ukumbi wa mikutano wa Redio Jamii Micheweni Shamata amesema  kudhibitiwa bandari hizo itakuwa ni moja ya njia ya kuwalinda vijana na makundi maovu .
Amesema  kuwa kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 ni kuhakikisha wananchi wote wanaishi kwa amani na utulivu , hivyo ni jukumu la watendaji  wa Chama hicho ngazi ya Matawi hadi jimbo kuandaa utaratibu wa kudhibiti bandari bubu ili zisitumike kinyume na taratibu .
“Sipendi kuona wala kusikia bandari bubu katika Jimbo langu zinatumika kupitishia dawa za kulevya pamoja na magendo , hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha mnakuwa mstari wa mbele kusimamia na kudhibiti matumizi yasiyo sahihi ”alieleza.
Aidha akizungumzia suala la uchaguzi  ndani ya Chama hicho , Shamata amewata kuachana na makundi baada ya uchaguzi katika matawi yao bali wawe wazalendo wa kukitetea na kukilinda chama kwa kuweka mbele maslahi ya umma.
Amesema kumbukumbu zinaonyesha kwamba wakati wa uchaguzi huwa kuna makundi ya wagombea na kuwataka kuyavunja makundi hayo na kushirikiana  katika kukijenga chama kwa kila mmoja kuhakikisha anashiriki kutafuta wanachama wapya.
“Makundi ni jambo lisilo epukika wakati  wa uchaguzi , lakini  yanahitaji  kuvunjwa baada  ya uchaguzi kumalizika kwani wote tuko ndani ya zizi moja na tunajenga nyumba moja ambayo ni Chama Cha Mapinduzi ”alisisitiza. 
Naye Zainab Salum  amesema matumizi hasi ya bandari bubu yamekuwa na athari kubwa kwa vijana ambao baadhi yao wamejiingiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya yanayopitishwa na kuingizwa nchi kupitia bandari hizo.
Amesema ni vyema wajumbe wa kamati  za saisa pamoja na wanachama wengine  kuondoa tofauti za za kisiasa , dini wala majimbo katika kufanikisha azma hiyo ili kuwalinda vijana dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kupitisha wahamiaji haramu .
Kwa upande wake Diwani wa wadi ya Kiuyu Ali Mkasha Mpemba ameitaka Serikali kujipanga kwa ajili ya kujenga kituo cha KMKM katika bahari ya Kiuyu ambayo huutmiwa zaidi na watu kupita  na kuingia nchi kinyume na sheria .

No comments