Header Ads

Responsive Ads Here

NAKURU TIMU YA TATU TOKA KENYA KUTINGA NUSU FAINALI SPORTPESA SUPER CUP,YAIBUTUA SIMBA YA TANZANIA


unnamed
 Kiungo wa Simba Mwinyi Kazi Moto (kulia) akiwania mpira na Amani Kyata, wa Nakuru All Stars,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

1
Beki wa Nakuru All Stars, Amakanji Ekuba, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba Sc, Juma Luizio, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
2
Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio (kulia) akichuana na Beki wa Nakuru All Stars, Amakanji Ekuba, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
3
Beki wa Simba, Mwambeleko Jamal (kushoto) akiwania mpira na beki wa Nakuru All Stars, Nandwa Sosi,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
4
Beki wa Nakuru All Stars, Mukhwana Sadicky, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Juma Luizio,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
6
Beki wa Nakuru All Stars, Mukhwana Sadicky, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Juma Luizio,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
7
Kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Nakuru,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
8
Winga wa Simba, Jamal Mnyate, (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Nakuru All Stars,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
9
Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto, akijipinda kupiga shuti kuelekea langoni kwa wapinzani, Nakuru All Stars,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
10
Beki wa Nakuru All Stars, akiokoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Mohamed Ibrahim,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Picha kwa hisani ya Montage Ltd
…………………………………….
Mchezo wa pili wa Michuano ya SportPesa umemalizika kwa Nakuru All Stars kuibuka na ushindi wa jumla ya Penalti 5-4 mchezo uliomalizika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kwa matokeo hayo timu ya Nakuru inayocheza Ligi daraja la kwanza nchini Kenya imetinga hatua ya Nusu Fainali ambapo watakutana na Goria Mahia toka Kenya waliofuzu baada ya kuwafunga Jang’ombe boys Jumla ya mabao 2-0.
Michuano hiyo itaendelea siku ya Alhamis kwa mechi mbili kupigwa mchezo wa Mapema utawakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga watakaocheza na AFS Leorpads na ya pili itakuwa kati ya Goria Mahia na Nakuru pia ya Kenya kwa hiyo Kenya wameingiza timu tatu kwenye Nusu Fainali na bingwa wa Michuano atacheza na Everton ya Uingereza July 13 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

No comments