Header Ads

Responsive Ads Here

NAIBU WAZIRI ANTHONY MAVUNDE AKUTANA NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA MJINI DODOMA


MKAO01Naibu waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg. Anthony Mavunde leo amefanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma juu ya namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.

Balozi Mattli ameupongeza mpango wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.
Balozi Mattli ameahidi kushirikiana na Serikali katika  kuunga mkono juhudi za Wizara katika uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha Shilingi 34,000,000 USD kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini
MKAO1

No comments