Header Ads

Responsive Ads Here

MWENGE WA UHURU WATEMBELEA MIRADI ILIYOGHARIMU BIL.2.596 KIBAHA VIJIJINI


unnamed
MKURUGENZI wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Tatu Seleman akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa mji wa Kibaha Jennifer Omolo .(picha na Mwamvua Mwinyi)

1
KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu ,Amor Hamad akisalimiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Tatu Seleman (picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha Vijijin
Mwenge wa Uhuru umetembelea miradi ya maendeleo nane yenye thamani ya sh.bilioni 2.596.1,katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha, mkoani.
Aidha mwenge huo ,ukiwa halmashauri ya Mji wa Kibaha ulitembelea miradi 10 yenye thamani ya sh .bilioni 13.775.965 .
Akikabidhi mwenge wa uhuru kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Tatu Seleman ,June 7 mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha Jennifer Omolo ,alieleza mji huo unapanuka kutokana na viwanda vilivyojengwa kwa wingi .
 
“Mkoa una zaidi ya viwanda 284 ambapo viwanda vinavyojengwa Mji wa Kibaha vitakuwa 103 wakati vikikamilika na utakiwa unaongoza kimkoa ” alisisitiza Jennifer.
 
Nae Tatu Seleman alisema,wanapambana na vitendo vya rushwa ,madawa ya kulevya pamoja na ugonjwa wa malaria na maambukizi mapya ya ukimwi .
 
Akizungumza katika viwanja vya shule ya msingi Uhuru iliyopo kata Janga ,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Amor Hamad ,aliwataka wananchi Kibaha waache kukaa kimazoea bali wafanye kazi.
 
Alikemea tabia ya baadhi ya watu ya kushinda kwenye ma-bar , kucheza pool na badala yake wajitume ili kupiga hatua kimaendeleo .
 
Amor alieleza, ni wakati wa kufanyakazi kwa bidii kwa kila kundi ikiwemo wakulima ,watumishi wa umma ,vijana ,wazee na wanawake .
 
Alieleza kuwa ,serikali inatia msukumo kwenye kukimbilia uchumi wa kati hivyo ni vyema kila mtu asiye na uwezo akajikita kuanzisha shughuli ndogondogo .
 
Hata hivyo ,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,aliwapongeza wajasiriamali wa Mji wa Kibaha kwa kuendana na kipaombele cha serikali cha kukuza uchumi .
Amor aliipa big up wilaya ya Kibaha kwa kusheheni viwanda na kushauri vitumike kutoa ajira mbalimbali .
Awali akizindua kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadala Vikige na kupanda miti ,alitoa rai kwa mmiliki wa kiwanda hicho kuweka nembo kwenye bidhaa hiyo ili kujitangaza .
 
Alisema kwamba ,endapo bidhaa mbalimbali zikiwekwa nembo zinazoonyesha utambulisho kuwa imetengenezwa wilaya ama mkoa husika na itatanua wigo wa kutambulika zaidi pia kuinua pato la halmashauri.
 
Katika hatua nyingine ,aliitaka jamii kulinda mazingira na kuacha kukata miti ovyo .
 
“Mkakati uliopo ni kupanda miti na kupiga vita uharibifu wa mazingira ili kulinda uoto wa asili ” alisema.
 

No comments