Header Ads

Responsive Ads Here

Muhimbili Yamtia Mbaroni Daktari Feki


DK FEKI
Kulia ni daktari feki ambaye amekuwa akijitambulisha kwamba ni Dk Abdallah Juma ambaye amekuwa akifanya kazi katika Maabara Kuu, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni mmoja wa askari wa Muhimbili aliyemkamata daktari huyo.


 Hospitali  ya Taifa Muhimbili (MNH) imemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwamba anaitwa Dk Abdallah Juma.
Mtu huyo alikuwa akijifanya kutoa huduma katika Maabara Kuu. Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa kijana huyo ni daktari feki na si daktari kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.
Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa walinzi walikuwa wakimtilia shaka na kuanza kumfuatilia hadi walipofanikiwa kumkamata.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye amekamatwa leo.

No comments