Header Ads

Responsive Ads Here

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI WILAYANI MAGU.


msangii-1
TAREHE 11.06.2017 MAJIRA YA SAA 14.30HRS KATIKA KIJIJI CHA WAMAGOLI KATA YA KABILA TARAFA YA NDAGALU WILAYA YA MAGU MKAO WA MWANZA, KASHELE MANOTA, MIAKA 81, MKAZI WA KIJIJI CHA WAMAGOLI, ANASHIKILIWA NA JESHI POLISI KWA KOSA LA KUPATINA NA NYARA ZA SERIKALI AMBAZO NI NGOZI YA KIBOKO, MIKIA MIWILI YA NYUMBU, NGOZI YA CHATU, JINO LA NGURUWE PORI NA NGOZI YA NYEGERE, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.

AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA KIJIJI TAJWA HAPO JUU YUPO MTU MWENYE NYARA ZA SERIKALI, KUTOKANA NA TAARIFA HIZO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI KIJJINI HAPO NA KUFANYA UPELELEZI NDIPO BAADAE ASKARI WALIWEZA KUBAINI MAHALI ANAPOISHI MTUHUMIWA KISHA KUINGIA NA KUFANYA UPEKUZI NYUMBANI KWAKE NA KUWEZA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA NYARA HIZO ZA SERIKALI.
POLISI WAPO KATIKA UPELELZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMNI. AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA SHUGHULI ZA UHALIFU WA AINA KAMA HII BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA KWAMBA KUMILIKI  NYARA ZA SERIKALI NI KOSA KISHERIA NA ENDAPO MTU ATABAINIKA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments