Header Ads

Responsive Ads Here

MSUVA AIPELEKA ROBO FAINALI COSAFA ‘TAIFA STARS’


Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetinga hatua ya  Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) Castle baada ya sare ya 1-1 na Mauritius jioni ya leo Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.

 
 Simon Happygod Msuva aliyetokea benchi kipindi cha pili na kwenda kuifungia Taifa Stars bao la kusawazisha dakika ya 68, dakika moja tu baada ya Kevin Perticots aliyetokea benchi pia kuifungia bao la kuongoza Mauritius.
Kwa matokeo hayo, Tanzania inaungana na Botswana, Zambia, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland zilizoanzia hatua hiyo na watamsubiri mshindi wa Kundi B kesho kukamilisha ‘Nane Bora’ za COSAFA 2017.
Na hiyo ni baada ya kumaliza na pointi tano sawa na Angola, lakini Taifa Stars inabebwa na wastani wake mzuri wa mabao, huku Mauritius na Malawi zote zikimaliza na pointi mbili kila moja.
Kundi B hadi sasa, Zimbabwe inaongoza kwa wastani wa mabao tu, ikiwa na pointi nne sawa na Madagascar, wakati Msumbiji ina pointi tatu na Shelisheli haina kitu.   
Mauritius leo ilimaliza pungufu baada ya mchezaji wake, Damien Balisson kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 78, lakini Tanzania ikashindwa kutumia mwanya huo kuongeza mabao.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Aishi Manula, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Abdi Banda, Salim Mbonde, Erasto Nyoni, Himid Mao, Shiza Kichuya, Elias Maguri/Simon Msuva dk58 na Thomas Ulimwengu.

No comments