Header Ads

Responsive Ads Here

MCHAKATO WA UCHAGUZI LIPULI FC


LIPULI 2014-15
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Juni 10 na 11, 2017 pamoja na mambo mengine ilijadili suala la uchaguzi wa Klabu ya Lipuli ya Iringa ambao awali ulipangwa kufanyika Mei 29, mwaka huu.

Hata hivyo, mchakato wa uchaguzi ulisitishwa na Kamati ya Uchaguzi uchaguzi ya TFF ambayo iliamua kufuatilia taratibu mbalimbali, kanuni na sheria na kujirisha kuwa unaanza upya kuanzia Juni 27, mwaka huu.
Uchaguzi huo sasa utafanyika Agosti 5, mwaka huu utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kama ilivyopangwa awali.
Uamuzi huo umezingatia malalamiko yaliyoletwa na wanachama ambao baadhi ya majina yaliyondolewa kwenye daftari la usajili la wanachama.
Tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF iko Iringa kwa ajili ya kutangaza rasmi uchaguzi huo ambako zoezi la kuchukua na kurejesha fomu litaanza Juni 28, mwaka huu.

No comments