Header Ads

Responsive Ads Here

MBUNGE KOKA ACHANGIA MILIONI 3 KWA AJILI YA UJENZI WA OFISI YA WAISLAMU WILAYA YA KIBAHA


KOKA1
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu hawapo pichani wakati wa sherehe za  Baraza kuu la waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Kibaha kwenye viwanja wa Mwendapole Wilayani Kibaha (PICHA NA VICTOR MASANGU)

KOKA2
Naibu Sheikh wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa  akizungumza jambo wakati wa sherehe hizo za baraza kuu la waislamu Wilaya ya Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………………………
VICTOR MASANGU, KIBAHA
VIJANA wa dini ya kiislmamu   hapa nchini wametakiwa  kuachana na vitendo vya kushinda vijiweni na kujiingiza katika wimbi la  uhalifu na utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo yanachgangia kwa kisi kikubwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa na badala yake  sasa wawe wazalendo kwa kuhakikisha wanazilinda  kwa hali na mali rasilimali zote pamoja na kutunza  amani iliyopo
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Sheikh wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa wakati wa  sherehe za baraza kuu la waislamu la Iddy  ngazi ya Wilaya ya Kibaha ambalo limefanyika katika viwanja vya mwendapole na kuhudhuliwa na  viongozi wa ngazi mbali mbali wa dini pamoja na serikali  kutoka katika Mkoa wa Pwani.
Sheikh Mtupa mbaye pia ni Kadhi wa Mkoa wa Pwani alibainisha kuwa kwa sasa watanzania wote wanapaswa kubadilika na   kuhakikisha kwamba wanakuwa walinzi wa rasilimali zote zilizopo nchini  kwa lengo la kuweza kuwathibiti baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijinufaisha wao wenyewe kwa maslani yao  binafsi bila ya kujali wananchi wa hali ya chini.
Hama kwa upande  wake Mbunge wa  jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo amewaasa wananchi wote  kuunga mkono  juhudi zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli  pamoja na kuchapa kazi kwa bidii ili kuweza kupambana na  janga la umasikini na kuachana na kuwa tegemezi ambapo pia amechangia kiais cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya waislmau ya  Wilaya.
Koka alisesema kwamba nia yake kubwa ni kushirikiana na wananchi wa jimbo lake katika kuleta maendeleo hivyo amewaomba waislamu waendelee kujenga upendo na ushirikiano wa hali na mali katika kuakikisha kwamba ujenzi wa ofisi hiyo ya wilaya inakamilika ili iweze kuanza kufanya kazi kwa jili ya kutoa huduma.
“Mimi kama mbunge wenu katika hili kwa kuanzia nitachangia kiais cha shilingi milioni tatu lakini sio kwamba ndio nitaishia hapo hapana nataka kuona na nyinyi wenzangu tunashirikiana kwa pamoja ili kuweza kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Wilaya na nikiona kwamba tupo pamoja na mimi tena nitaongezea kiasi cha shilingi milioni mbili lengo ikiwa ni kuona tunakuwa na sehemu sahihi ya kuweza kukutana na kufanya shughuli zenu,”alisema Koka.
Awali akisoma risala katika sherehe hizo  Katibu wa kamati ya maandalizi ya Baraza la Iddi Wilaya ya Kibaha  Hoseni Ibrahimu ameiomba serikali ya awamu ya tano  kuongeza vipindi vya dini mashuleni kwa lengo la kuweza kutoa huduma za kiroho kwa wanafunzi wa kiislamu
“sisi kama baraza kuu la waislmamu Bakwata Wilaya ya Kibaha kikubwa tunachoiomba serikali ni kuongeza vipindi vingi vya dini katika mashule ili wanafunzi waweze kupata fursa ya kujifunza zaidi mafundisho ya kiroho na tuna imani itaweza kusaidia kuwaongezea uwezo mkubwa katika kujifunza mambo mbali mbali yanayohusina na dini ya kiislamu,”alisema Ibrahimu.
BARAZA kuu la waislamu (BAKWATA)  Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani  kwa sasa licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali   linahitaji kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya  ujenzi wa ofisi ya wilaya.

No comments