Header Ads

Responsive Ads Here

‘MASHEMEJI DERBY’ KIVUTIO CHA AINA YAKE SPORTPESA SUPER CUP FAINALI YAKE JUMAPILI UWANJA WA UHURU


IMG_0334
Baada ya mechi za nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2017 tumeshuhudia timu zote za Kenya zikifuzu kucheza fainali huku fainali ikiwa ni mechi ya wapinzani wakubwa wa soka la Kenya AFC Leopards vs Gor Mahia.

Bahati tuliyopata wadau wa soka nchini ni kuishuhudia ‘derby ya mashemeji’ AFC Leopards vs Gor Mahia, mechi hii ni kama Simba na Yanga zinapokutana.
Gor Mahia na Leopards ni timu washindani wa siku nyingi sana kwenye soka la Kenya, ni timu ambazo upinzani wao unatokana na historia ya makabila makubwa ya nchini Kenya. Upinzani umekuwa mkubwa kiasi cha timu nyingine zikazipa changamoto hati timu hizi zikashuka daraja na kupotea kwenye ramani ya soka kabla ya kujipanga na kurejea upya.
Gor Mahia imekuwa ikifanya vizuri sana siku za karibuni kwenye ligi ya Kenya sambamba na AFC Leopards na matokeo yake yakaleta tena vuguvugu la upinzani.
Kama umekuwa ukifuatilia derby hii hata kupitia vyombo vya habari, katika miaka ya hivi karibuni timu hizi kila zinapokutana mechi zimekuwa hazimaliziki salama, lazima utokee ‘mtiti’ au mechi kusimama kwa dakika kadhaa ili vurugu na fujo zitulizwe.
Tunataraji kuiona darby nchini ikiwa ni mechi ya fainali ya michuano ya SportsPesa Super Cup, lakini tujiulize swali, kati ya timu nne za Kenya timu tatu ziliingia nusu fainali na timu mbili zimefika fainali je soka la Kenya lipo juu kuliko Tanzania au kwa sababu vilabu vya Tanzania havikuwa na wachezaji wao wengi wa vikosi vya kwanza?
Kocha wa zamani wa Ndanda na Azam, mtanzania Dennis Kitambi amesema ni nafasi kwao kurudisha kisasi kwa Gor Mahia ambao waliwafunga goli 3-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Kenya.
“Hata wakati tunaondoka Kenya watu wengi walikuwa wanatumaini fainali itakuwa ni ‘Mashemeji Derby’ katika nchi ya ugenini kwa hiyo na sisi tulikuwa tunaombea tucheze dhidi ya Go Mahia kwa sababu kwetu itakuwa nafasi ya kurudisha goli tatu walizotufunga kwenye ligi,” Dennis Kitambi.
Kwa upande wa kocha wa Gor Mahia amesema, anaamini timun yake itashinda mechi hiyo kwa sababu siyo mara ya kwanza anakutana na AFC Leopars.
“Mechi tuliyocheza na Leopards ilikuwa ni ligi na tulikuwa tukihitaji pointi tatu, tulipata na tulifurahi sana sisi wote tutakuwa tunataka kushinda lakini kitu kikubwa ni kwamba sifikirii kama ni mechi ngumu kwa sababu niliwafunga 3-0 nikiwa kocha mkuu.”

No comments