Header Ads

Responsive Ads Here

MASAUNI, IGP SIRRO WAWATAKA WANANCHI WILAYA YA KIBITI,RUFIJI KUFUNGUKA DHIDI YA VITENDO VYA UHALIFU NA WAHALIFU


unnamed
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bungu, wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani, kuhusiana na masuala mbalimbali ya kupambana na wahalifu wilayani humo. Masauni ambaye aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwasambaratisha wahalifu hao


1
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipokea maoni ya wananchi wa Kijiji cha Jaribu Mpakani wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi wilayani humo. IGP ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) walizungumza na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
2
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu (hawapo pichani) kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti kuhusu masuala mbalimbali na  kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, na kushoto ni Mkuu wa Wilaya Kibiti, Gulam Hussein. 
3
Wazee, viongozi wa dini na wa vyama vya siasa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari ya Kibiti, mkoani Pwani. Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro pamoja na wananchi hao waliweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao kupitia maoni ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments