Header Ads

Responsive Ads Here

Marafiki wa Bahari Washerehekea Siku ya Bahari Duniani Kwa Usafi


unnamed
Marafiki wa Bahari kutoka Mikocheni B, kwa kushirikiana na wadau wengine wakishiriki zoezi la kufanya usafi kati ufukwe wa bahari ikiwa ni kusadhimisha siku ya Bahari Duniani leo Jijini Dar es Salaam.
1
Marafiki wa Bahari kutoka Mikocheni B, kwa kushirikiana na wadau wengine wakicheza mpira mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi kati ufukwe wa bahari ikiwa ni kusadhimisha siku ya Bahari Duniani leo Jijini Dar es Salaam
………………………………..
Na: Mwandishi Wetu
Marafiki wa Bahari kutoka Mikocheni B wakidhaminiwa na Alternative radio 92.9fm ya mjini Dodoma pamoja na Kampuni ya Koncept Communication wamefanya usafi katika  fukwe za Mikocheni B leo katika kuunga mkono utekelezwaji wa kipengele cha 14 cha Malengo 17 Endelevu ya Agenda ya Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa kikilenga kuendeleza uhai katika maji, kuongeza uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.
Katika zoezi hilo jumla ya taka zilizookotwa ni Chupa 450 za maji; mifuko 150 ya chakula(foil); makopo 1554 ya bia, chupa 2000 za bia, nguo 74, viatu 600, matairi 12,vizibo i560 , midoli 24, vyombo vya jikoni, nyavu 6 na vipisi vya sigala 500.
Tarehe 8 Juni kila mwaka ni siku ya kusherekea na kuungana kwa pamoja katika fukwe za bahari na kusafisha kama jitihada za maendeleo ya baadae na kufikia lengo la kuendeleza uhai katika maji na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Bahari Yetu, Maisha Yetu ikihamasisha kutatua tatizo la uchafu sugu wa plasitiki, viwandaani, uvuvi haramu na mabadiliko ya tabia ya nchi ikihatarisha uhai wa bahari na maisha ya baadae.
Leo miji yote duniani iliyo pwani inaadhimisha kwa kukusanyika katika fukwe huku wakisherehehekea kwa matukio mbali mbali  na kushiriki katika zoezi la kusafisha fukwe wakiokota uchafu sugu.
Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo jumatatu tarehe 5 Juni,Katibu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutterres amesema ni lazima kutafsiri utashi wa kisiasa wa Ajenda ya mwaka 2030 , Mkataba wa Paris wamazingira na Ajenda ya Addis Ababa kateshwa kiedha.
Siku hii imekuja wakati kongamano la kwanza kabisa la bahari kuwahi kutokea duniani likiendelea kwa siku ya 3 sasa huko mjini new York nchini marekani na kuisha  kesho ijumaa tarehe 9 Juni. Kongamano hili linategemewa zaidi katika kutoa wito wa kuchukua hatua ili kuiokoa bahari.
Guterres aliongeza kuwa atahakikisha amevunja vizuizi vyote kati ya Umoja wa Mataifa, Miradi ya maendeleo katika kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji katika kufikia malengo ifikapo 2030.
Kongamano hili linaonekana kuwa ni la umuhimu sana katika kupata mbinu na njia mbadala za kutatua tatizo la uchafu sugu wa plastiki, ongezeko la acidi baharini kutoka, uvuvi ulio kithiri wa uwezo wa bahari na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayo hatarisha uhai wa bahari.
Washiriki kutoka katika Serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na jumuiya ya wanakisayansi wakishiriki kongamano. Waziri wa Mifugo, Kilimo na Uvuvi Dkt. Chares Tizeba akiongoza ujumbe kutoka Tanzania katika kuunga mkono mkakati wa utekelezwaji wa kipengele cha 14 cha Malengo 17 Endelevu ya Agenda ya Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa kinacho lenga kuendeleza uhai katika maji, kuleta uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.
Kwa upande wake Mjumbe wa Serikali za Mtaa wa Mikocheni B, Moses Sanga amesema kuwa jamii inapaswa kupunguza kutumia plasitiki kwa matumizi ya maramoja kama chupa za maji, mifuko navinginevyo ili kupunguza kiwango cha biaadhaa za plasitiki kinachoingia baharini,
Tafiti zinaonyesha kuwa takribani tani million nane za taka zitokanazo na bidhaa za plastiki huingia baharini kila mwaka jambo linalotoa tafsriri ya kwamba ifikapo mwaka 2050 plastiki zitakuwa nyingi zaidi kuliko samaki na viumbe vingine vya baharini.
Pamoja na shughuli hii kufanyika leo, inatarajiwa kufanyika rasmi siku ya Jumamosi ya tarehe 10 Juni ambapo asasi za kiraia za Nipe Fagio, Mbezi Beach Neighborhoods, Marafiki wa Bahari kutoka Mikocheni B, pamoja na wadau wengine kutoka Serikali, mashirika binafsi, wafanyabiashara na watu binafsi wakifanya fukwe kuwa safi huku wakisherehekea kwa shamlashala mbalimbali. Watu wote wanakaribishwa kutumia fursa hii kujifunza mengi kuhusu katika jitihada za kufikia malengo ya 2030 ya umoja wa mataifa kwa manufaa ya wote.

No comments