Header Ads

Responsive Ads Here

KIMENUKA; MALINZI, MWESIGWA, KABURU WAPELEKWA RUMANDE


malinzi jela
Rais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais kwa kuwa amepelekwa mahabusu katika Gereza la Segerea baada ya kukosa dhamana hadi Jumatatu Julai 3 kesi yake itakaposikilizwa tena.
Malinzi pamoja na Katibu wake, Mwesigwa Celestine wanashitakiwa kwa makosa 28 yakiwemo ya kugushi na utakatishaji fedha.
Wote wawiliw amepandishwa gari kwenda Segerea hadi Jumatatu kesi yao itakaposikilizwa tena.
Pamoja na wao, Rais wa Simba,  na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ wanaoshitakiwa kwa makosa ya utakatishaji, nao wamechukuliwa kupelekwa Segerea.
Kaburu na Aveva watakuwa mahabusu hadi Julai 13 baada ya kukosa dhamana kutokana na kesi inayowakabiri.

No comments