Header Ads

Responsive Ads Here

KAMPUNI YA MAXCOM AFRIKA YATOA WITO KWA MAKAMPUNI NCHINI KUUZA MITAJI KATIKA SOKO LA HISA ILI KUKUZA UWEKEZAJI.


unnamed
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika (Max Malipo) Dkt.Donalth Ulomi akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari wakati wa kutambulisha hati itakayoiwezesha  kampuni hiyo kuuza hisa zake kwa umma  Jijini Dar es Salaam.

1
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika (Max Malipo) Dkt.Donalth Ulomi (kulia) akifafanua jambo  wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Kampuni hiyo  ilitambulisha hati itakayoiwezesha   kuuza hisa zake kwa umma  Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Msimamizi Bw.Ahemed Lussasi.
2
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika (Max Malipo) Dkt.Donalth Ulomi(kushoto) na Mkurugenzi Msimamizi wa Kampuni hiyo Bw.Ahemed Lussasi wakionyesha bango jipya la kampuni hiyo katika mkutano wa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.(Picha na Mpiga Picha wetu).
……………………
Na Mwandishi Wetu
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika (Max Malipo) Dkt.Donalth Ulomi ametoa wito kwa makampuni nchini kuuza  mitaji yao katika soko la Hisa ili kutimiza adhama ya Serikali ya kupanua wigo wa umiliki wa makampuni.
 Dkt.Ulomi aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Kampuni hiyo ilipata fursa ya  kutambulisha hati itakayoiwezesha  Maxcom kuuza hisa zake kwa umma.
“Leo kampuni yetu imetoa hati rasmi inayotambulisha  Maxcom Afrika kuwa moja ya kampuni inayomilikiwa na umma, ambapo ni hatua nzuri kwetu na fursa kwa wananchi wa kitanzania kuwekeza kupitia manunuzi ya hisa”alisema Dkt.Ulomi.
Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa hatua hiyo ni katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ambapo ameyataka makampuni nchini kuuza asilimia 25 ya hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Dkt. Ulomi amezidi kufafanua kuwa  kampuni hiyo ipo katika hatua za  kukamilisha mchakato wa kubadili jina na kuwa Maxcom Afrika Public Limited Company (Maxcom Africa Plc) ambapo kwa sasa  inangojea kibali cha wasimamizi wa soko la hisa ili iaanze kuuza mara moja kwa watanzania watakaokuwa tayari kuwekeza.
 Maxcom Afrika PLC ni kampuni iliyoanzishwa na vijana wazawa wa kitanzania na imefanikiwa kutoa ajira takribani 449 moja kwa moja kwa zaidi ya watanzania elfu 16 huku ikiwa na lengo la kutoa ajira laki moja ifikapo mwaka 2020.

No comments