Header Ads

Responsive Ads Here

GS WARRIORS BINGWA MPYA NBA,WAITANDIKA CLEVELAND 129-120


NBA-8

KEVIN DURANT alikuwa katika kilele cha umahiri wake kwa kuisaidia timu yake ya Golden State Warriors kutwaa ubingwa wa Ligi ya Basketball ya Marekani (NBA) dhidi ya mahasimu wao Cleveland Cavaliers katika mchezo uliomalizika alfajiri ya leo kwa saa za Afrika Mashariki.

Mchezaji huyo alifunga pointi 39 katika mchezo wa vuta-nikuvute uliomalizika kwa ushindi kwa pointi 129 kwa 120.
Stephen Curry aliongeza point 34, pasi za mwisho 10 na mipira sita aliyoitumbukiza kwenye neti baada ya kugonga ubao.  Warriors walijihakikishia ushindi huo kufuatia kushinda mchezo wa saba wa mfululizo wa 4 kwa 1, hivyo kunyakua tena ubingwa wake wa pili katika miaka mitatu baada ya kushindwa kwa 3 kwa 1 mwaka uliopita.  

No comments