Header Ads

Responsive Ads Here

DTB BENKI KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZAO MKOANI TANGA


 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine
Shigella akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB kwa
ajili ya wateja wao mkoani Tanga  iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga
Beach Resort,kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu na kushoto ni
Meneja wa Benki ya DTB Mkoani Tanga,Athumani Juhudi
 MKUU wa wilaya ya
Tanga,Thobias mwilapwa akizungumza wakati wa futari
hiyo
Shehe wa Mkoa wa
Tanga,Juma Luwuchu akitoa neno kwenye futari hiyo
 Meneja wa
Benki ya Diamond Trust Bank
Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi akizungumza na waandishi wa
habari
Wageni waalikw
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi
Mayeji kushoto akisalimiana na Aliyekuwa Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj
Kassim Kisauji wakati wa hafla ya futari hiyo
 sehemu ya wageni waalikwa
wakipata futari

BENKI ya Diamond Trust(DTB)
Tawi la Tanga wanakusudia kupanua wigo wa huduma zao kwa wateja kwa kukarabati na kuongeza
namba ya wahudumu ikiwa ni
mkakakti wa ujio wa fursa mbalimbali mkoani hapa ukiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta
kutoka hoima nchini Uganda hadi
Bandari ya Tanga.
Hayo yalibainishwa juzi na Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi
wakati futari iliyoandaliwa na
Benki hiyo kwa wateja
wao wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Tanga Beach Resort mjini hapa na kuhu
dhuiwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo wakuu wa wilaya za Handeni na Tanga.
Alisema wao wanakusudia kufanya hivyo ili kuweza kuendana na wigo mpana wa ukuaji wa uchumi kwa mkoa
wa Tanga ambao unatarajiwa
kufanyika kutokana na mradi huo mkubwa .
“Benki yetu ipo kwenye nafasi ya tano kati ya mabenki zenye amana kubwa za wateja hivyo tumeona
kuwaandalia futari hiyo ni namna bora ya kuwashukuru wao kwa kuwasapoti”Alisema.
“Unajua wateja wetu wamekuwa wakitusapoti hivyo ndio maana
tumeona vizuri kuwaandalia
futari lakini pia niwaambie kuwa  wanaweza kutuma na  kusafirisha fedha kwa
haraka kutoka nje ya nchi na ndani ya
nchi”Alisema
Awali akizungumza katika hafla hiyo,Mkuu  wa Mkoa wa
Tanga,Martine Shigella
aliwataka wakazi wa mkoa huu kuendelea kumuombea Rais John Magufuli aweze kuendelea kupigania
haki za watanzania wanyonge ambazo
zimekuwa zikipotea.
Alisema kuwa kiongozi huyo mkuu wa nchi amekuwa akifanya mambo
makubwa ya kuhakikisha
watanzania wanapata maendeleo haraka na kukuza uchumi ambao utatufikisha kwenye
mafanikio.
“Ndugu zangu waislamu tuendelee kuombea nchi yetu na Rais wetu
ili yeye na viongozi wote
waendelee kutenda yaliyomema na yanayompendeza mwenyezi mungu”Alisema RC Shigella.
“Lakini pia niendelee kuwashukuru kwa kuendelea kudumisha amani
na mshikamano kwa mkoa huu kwa
kipindi cha tokea mwezi ulipoanza mpaka sasa  hivyo muendelee kuwa na upendo kwa watu
wote.
Awali akizungumza katika futari hiyo,Shehe wa Mkoa wa Tanga, Juma Luwuchu  aliwataka waislamu
mkoano hapa kuendelea mshikamano waliokuwa nao kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa
kuendelea kutenda yaliyo
mema.
“Tuendelee kushikamana tupendane lakini kubwa zaidi tuhakikisha tunazingati kufanya ibada mara kwa
mara na sio kipindi cha mwezi huutu hata baada ya kumalizika kwake
“Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha

No comments