Header Ads

Responsive Ads Here

Dkt. Pallangyo akutana na Watendaji kutoka Benki ya Dunia


Na Rhoda James

Leo Juni 23, 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amekutana na Watendaji kutoka Benki ya Dunia (WB) waliomtembelea kwa ajili ya kupata taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali ya madini inayotekelezwa na Wizara. Kati ya masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na uimarishaji wa Sekta ya Madini, Mafanikio ya miradi yake pamoja na taasisi.
MWASE1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (mbele) akielezea miradi ya Sekta ya Madini na mafanikio yake. Wengine katika Picha ni Ujumbe kutoka Benki ya Dunia (WB), Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

MWASE2
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiwa katika kikao hicho.
MWASE3
Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Sudeshna Banerjee ( wa kwanza kulia) akielezea mipango walionayo katika kusaidia utekelezaji wa Miradi ya Sekta ya Madini ili iendane na Vipaumbele vya Serikali.

No comments