Header Ads

Responsive Ads Here

DK.MAGUFULI -“NITALALA NAO MBELE ,WAHUJUMU UCHUMI HADI WAKOME”KWA MASLAHI YA WANYONGE


1
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,dk.John Magufuli ,amesema anaendelea kula sahani moja na wapiga dili /wahujumi uchumi ,hadi watakapokoma ili kuondoa umaskini uliopo nchini.

Amesema yupo tayari kwa kazi hiyo licha ya kuwepo baadhi ya watu wanaouumia kutokana na utekelezaji wake na ameomba watanzania wanyonge wamruhusu afanyekazi kwa maslahi yao.
Aidha amesema uongozi wa mkoa wa Pwani umemkuna na kumfurahisha kwa kutekeleza azma ya awamu ya tano ya ujenzi wa viwanda na kukuza uwekezaji.
Dk.Magufuli ,amewataka viongozi mbalimbali wa serikali kujitathmini kwa nafasi walizonazo ndani ya miezi sita,mwaka na endapo itafika mika miwili kongozi husika akijiona hatoshi basi  ajiengue.
Katika hatua nyingine ,amewaomba wakazi wa Rufiji na Kibiti,kuwafichua wahalifu wanaoua baadhi ya viongozi na wananchi ili waweze kuendelea   kuwa na amani na maendeleo.
Wakati huo huo amesema wapo baadhi ya wakubwa wanaoingiza madawa ya kulevya na kuumiza watoto wa wanyonge hivyo ni lazima wachukuliwe hatua ili kukomesha hali hiyo na kuokoa nguvu kazi inayopotea.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uwanja wa Bwawani Mailmoja ,Kibaha wakati wa ziara yake ya kikazi ,aliyoianza mkoani Pwani,alisema Tanzania ni nchi tajiri lakini inakuwa maskini kutokana na wapigaji wachache wasioitakia mema.
“Wataula wachuya kwa uvivu wa kuchagua,nitawabana wezi wote ili hali tuweze kuondokana na usindikizaji wakati sie ni matajiri”
“Wezi ni wezi tuu,hata kama upo,hata kama kiongozi mla dili ni mwizi tuu,tumelaliwa vyakutosha ,tumechezewa sana hivyo sasa nipeni ruhusa nilale nao mbele ili tuweze kunufaika na raslimali zetu ”alisema rais Magufuli.
Alieleza tuna wajibu wa kuipeleka Tanzania mbele ili kuondokana na umaskini uliopo,haiwezekani kukosekane umeme,chakula ,tufe maskini ,ni lazima tutumie vya kwetu kujiongezea uchumi na kupiga hatua kimaendeleo.
Dk.Magufuli alieleza kwamba,yeye ni rais wa vyama vyote na hayupo kwa ajili ya chama ,bali wajibu wake ni kuwatumikia wananchi wote kwa manufaa ya wote bila kubagua itikadi za  kisiasa.
“Tanzania ina madini ya kila aina ,ikiwemo tanzanite lakini hayaisaidii Tanzania,Tunakila aina ya gesi ,na madini lakini tunakufa maskini na wananchi wanaoishi kwenye nchi hii wanakufa maskini,”Tuna maziwa zaidi ya 21 tunaweza kuvua samaki lakini angalia maisha yetu ,mbunga za wanyama asimilia 25 ni hifadhi ya taifa  ,watu wanakuja kutalii na kupata mapato lakini hakuna tunachopata”
“Tanzania ni watatu kuwa na mifugo mungu atupe nini,tuna mlima Kilimanjaro lakini hakuna kitu,lazima tujiulize tulikosea wapi”alisema dk.Magufuli .
Akizunumzia  yaliyofanyika hadi sasa Dk.Magufuli alibainisha kuwa,kuna sh .bilioni  18.77 zinatolewa kwa ajili ya watoto kusoma bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne kila mwezi.
 kwa ajili ya mashule walimu wasinhezipata ,ili isiwepo mahala pa kupitapita 100000
Kutokana na fedha kupelekwa wameshaandikishwa wanafunzia mil.mbili kutoka mil.moja na wanafunzi wa shuleza sekondari wamefikia asilimia 27 na tayari kumeboreshwa miundombinu ya shule 1,700.
Dk.Magufuli alisema  upande wa madawa walitenga bilioni 31 ambapo kwasasa imefikia bilioni.250 huku mikopo ya vyuo vikuu ikifikia bilioni 473 kutoka bilioni 373.
Hata hivyo hakusita kuzungumzia sakata la mishahara hewa ambako wafanyakazi 19,000 walibainika kupokea mishahara feki kwa majina hewa .
Kufuatia mafanikio hayo,amewathibitishia wananchi wa Kibaha kuwa kila siku atakuwa upande wa wanyonge  na ataendelea kuwatetea wanyonge kwa kutimiza ahadi zote alizowaahidi wakati wa kampeni .
Nae mkuu wa mnkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema hadi sasa mkoa huo una viwanda 371 ambapo vikubwa ni 89 vidogo na vya kati  ni 260 na vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi .
Alisema licha ya kujipanga kuwa ukanda wa viwanda lakini wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara,kukosa maji na umeme wa uhakika na gesi.
Mhandisi Ndikilo ,alisema kuwa mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya wateja kuhitaji kuunganishiwa umeme lakini vifaa kama vile nguzo, mita na nyaya ni vichache,hivyo uongezewe nguvu ya umeme megawatt  60 ambapo kwasasa wanapata megawati 38 hadi 40 ambazo hazikidhi mahitaji.
Alisema megawatt zilizo pungufu ni  megawatt 20 kwa sasa ili kukidhi mahitaji bila umeme hawawezi kupata ukuaji wa uwekezaji .
Mhandisi Ndikilo ,alimuomba mh,Rais kutupia macho suala la kuwekalami katika barabara ya Kisarawe,Maneromango,Mlandizi kwani  itarahisisha usafiri na wawekezaji.
Alieleza barababa ya Kiluvya -Kisarawe yenye-km 19 itasaidia kupunguza msongamano  hivyop pia wanaomba zipitishwe na kuwa katika kiwango cha lami.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kibaha,Silvestry Koka, alisema wananchi wa Kibaha wanamuunga mkono juhudi za  rais Magufuli anazoendelea nazo na hatua ya kuinua uchumi kwa manufaa ya vizazi vijavyo .
Alieleza Mji wa Kibaha unakua lakini una changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara na barabara muhimu kushindwa kupandishwa hadhi ikiwemo barabara ya Tamco-Mapinga yenye km.24 na ya Kwa Matias kwenda kikosi cha ardhi Msangani.
Alieleza kwamba , Tamco -Mapinga ni miaka 12 iliyopita wananchi walisimamishwa wasiendelee na shughuli za kijamii na kinachokwamisha ni fidia kwa wananchi ya takriban mil .8.400 .
“Hii barabara inaahirishwa ahirishwa sana tunaomba mh .rais utusaidie kutukingia kifua ili ziweze kupatiwa lami na hatimae kurahisisha usafiri”alisema Koka.
Rais Magufuli,ameanza ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ,ambapo june 20 alizungumza na wananchi wa mji wa KIbaha,june 21 na 22 atazindua viwanda vitano vikubwa ikiwemo cha kusindika matunda,vifungashio,cha chuma,cha matrekta na kufungua kiwanda cha sayona.
Pia atazindua barabara ya Msata-Bagamoyo ili kuendelea kurahisisha usafiri na atafungua mradi wa maji-Ruvu.

No comments