Header Ads

Responsive Ads Here

Balozi wa Ujerumani Avutiwa na Mazingira ya Biashara Nchini


unnamed
Balozi mdogo wa Ujerumani nchini Balozi John Reyes (wa kwanza kulia) akiwa na sehemu ya wageni waalikwa katika hafla ya kupongeza kampuni za Kijerumani zinazoshiriki maonesho ya biashara ya kimataifa Sabasaba mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana jioni.

1
  Balozi mdogo wa Ujerumani nchini Balozi John Reyes (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka Ujerumani Bwana Bob Hooda (kushoto) na Ofisa Habari wa Ubalozi huo  Bwana John Menkion (kulia) nyumbani kwa balozi huyo jijini Dar es Salaam jana katika hafla ya kupongeza kampuni za Kijerumani zinazoshiriki maonesho ya biashara ya kimataifa Sabasaba mwaka huu.
2
Balozi mdogo wa Ujerumani nchini Balozi John Reyes (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka Ujerumani Bwana Bob Hooda (kushoto) na Ofisa Habari wa Ubalozi huo  Bwana John Menkion (kulia) nyumbani kwa balozi huyo jijini Dar es Salaam jana katika hafla ya kupongeza kampuni za Kijerumani zinazoshiriki maonesho ya biashara ya kimataifa Sabasaba mwaka huu.
……………………….
NA MWANDISHI WETU, DAR
BALOZI Mdogo wa Ujerumani nchini Balozi Joh Reyes amesema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayokua kwa sasa kiuchumi katika bara la Afrika hivyo kuvutia wawekezajiwengi kutokana na mazingira mazuri ya biashara.
Akizungumza nyumbani kwake jana katika hafla ya kupongeza kampuni zinazotangaza bidhaa a Kijerumani katika maonyesho ya kimataifa ya biashara jijini Dar es Salaam maarufu Sabasaba, Balozi Reyes alisema nchi yake inatazamia kuwekeza zaidi katikaardhi ya Tanzania.
“Kwa mara nyingine Ujerumani inapeperusha bendera yake katika maonyesho ya Sabasaba, hii ni ishara nzuri kuwa sehemu ya wawekezaji kwenye taifa linalokua kwa kasi kiuchumi. Katika Afrika Mahsariki na Kati pamoja na Afrika nzima Tanzania imeonyesha kukua kwa kasi.
“Kuna fursa nyingi za uwekezaji na ndiyo maana bidhaa kutoka Ujerumani zimekuwa zikiongezeka. Kampuni hii ya CFAO Motors inayouza magari mbalimbali ikiwemo Volkswagen na Mercedes Benz kutoka Ujerumani ni miongoni mwa kampuni zitakazoshiriki maonyesho haya, nwaomba mfike kwenye banda letu la Ujerumani muone bidhaa nyingi zaidi,” alisema Balozi Reyes.
Alisisitiza kuwa amani na nia ya dhati ya kukua kiuchumi ni miogoni mwa tunu zinazoifanya Tanzania kuazamwa kwa jicho zuri na mataifa yaliyoendelea kiviwanda. Hivyo atatumia nafasi yake kuhakikisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, kuwa na uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025 inatimia kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko cFAO Motors, Bibi Tharaia Ahmed akiwa katika ghafla hiyo alisema kampuni yao imekuwepo nchini tangu mwaka 1952 wakati huo ikiitwa DT Dobie, maana yake wanalitambua soko la Tanzania vizuri.
“Magari tunayoingiza nchini ni yale yaliyotengenezwa kutokana na mazingira ya kitanzania, tumekuwepo Tanzania tangu enzi za Tanganyika kwa zaidi ya miaka 60 tunahudumia watanzania. Tunajua huu niukanda wa vumbi hivyo tunaagiza magari yenye vifaa vya kuzua vumbi kuharibu gari pamoja na aina ya barabara zilizopo magari yetu yanastahamili,” alisema Bi. Tharaia.
Alibainisha kuwa watu wasiangalie gharama bali waangalie uwekezaji katika vyombo vya usafiri vinavyodumu na kustahamili mazingira magumu, ndiyo maana magari ya Volkswagen yapo aina mbalimbali ikiwemo za kubebea mizigo (Pick Up), za matumizi ya nyumbani na za kiofisi (Volkswagen Touareg) mabayo inastahamili barabara zote hadi mikoani.
Kwa upande wake mmoja wa wafanyabiashara mwenye asili ya Ujerumani anayeishi nchini Bwana Bob Hooda, kutoka kampuni ya WIPRO GmbH alisema kwa sasa Tanzania inaingia katika uchumi wa viwanda hivyo itahitaji umeme wa uhakika, miongoni mwa shughuli wanazofanya zinahusiana na umeme hivyo watatimiza wajibu wao.
“Mimi nimeishi Tanzania kwa miaka mingi nafahamu tupo katika kipindi cha kupaa kiuchumi, tunahitaji umeme wa uhakika utakaoendesha viwanda. Naomba mtembelee banda letu la Ujerumani pale viwanja vya Sabasaba ili muone shughuli tunazofanya kumuuunga mkono Rais John Magufuli,” alisema Bw. Hooda.

No comments