Header Ads

Responsive Ads Here

AZAM FC WATHIBITISHA KUONDOKA KWA MANULA NA KAPOMBE

Uongozi wa timu ya Azam FC umethibitisha taarifa ya wachezaji wake Aishi Manula na Shomari Kapombe kusajiliwa na mabingwa wa michuano ya FA timu ya Simba kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
Mwenyekiti wa klabu ya Azam Iddrisa Nassoro alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi wa klabu hiyo hawana kinyongo na wachezaji hao katika harakati za kuondoka kwao kwani ni moja ya kuendelea kusaka mafanikio kwa upande kwao.

Aidha Nassoro alisema kwamba uongozi unawashukuru wachezaji hao kwa ushirikiano wao ambao wameuonyesha tangu walipojiunga na Azam kwani kwa njia moja walifanikiwa kuipa maendeleo timu hiyo.

Alisema kwamba kwa sasa kwao wanaendelea kuifanyia kazi taarifa ya mwalimu mkuu kuhakikisha wanatimiza matakwa yake ikiwemo kusajili wachezaji ambao watakuwa na chachu ya mafanikio kwa klabu.
Kapombe-Azam
Kapombe na Manula wamejiunga na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili kwa kila mmoja huku ikielezwa kila mmoja amesajiliwa kwa dau la shilingi milioni 50.

No comments