Header Ads

Responsive Ads Here

AMOR – KILA MWANANCHI/ HALMASHAURI INA WAJIBU WA KUSAMBARATISHA MALARIA


unnamed
KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa 2017 ,akielezwa namna kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited kilichopo Kibaha Mkoani Pwani,kinavyozalisha bidhaa zake ,wa tatu kulia ,kaimu meneja masoko ,Frank Mzindakaya .
1
Kaimu mkurugenzi kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited kilichopo Kibaha Mkoani Pwani,Samwel Mziray akimkabidhi kiongozi wa mbio za mwenge taarifa ya kiwanda hicho .(picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WANANCHI na halmashauri nchini zimetakiwa kununua bidhaa zinazozalishwa Tanzania ikiwemo dawa za kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria zinazotengenezwa Kibaha ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
Amesema ni wakati wa watanzania kuwa wazalendo wa kupenda vyao kwani Tanzania ya viwanda ni kuangalia masoko ya bidhaa za ndani na kupiga vita vinavyozalishwa nje .
Kauli hiyo ilitolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2017 ,Amor Hamad Amor wakati alipokwenda kuzindua kampeni ya kudhibiti malaria Kibaha Mji na kutembelea kiwanda cha  kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited .
Alisema, dawa za kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria zinapaswa kununuliwa na kila halmashauri kutoka kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali kwa asilimia 100.
Hata hivyo ,Amor alieleza mpaka sasa mwitikio wa jamii na halmashauri hauridhishi .
“Tunajirejesha nyuma kimasoko lakini mkumbuke lengo la Serikali ni kupunguza vifo vitokanavyo na malaria nchini hasa kwa akinamama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano”, alisema Amor.
Alisema kwamba iwapo kama halmashauri hasa zilizopo Bara zitanunua dawa hizo na kuzitumia, ugonjwa huo utapungua kwa kiasi kikubwa na kuwa kama Zanzibar ambayo ugonjwa huo upo kwa asilimia moja.
Amor alielezea kuwa, kazi ya kupambana na malaria ni ya kila mmoja hivyo tupambane kwa kununua dawa hizo pasipo kujirudisha nyuma kimasoko . 
Alimpongeza Rais wa awamu ya nne ,dk.Jakaya Kikwete kwa kuwa chanzo cha kuwepo kiwanda hicho kwa lengo la kuhakikisha kwamba Tanzania inakua huru dhidi ya malaria .
” Niwahakikishie kuanzia sasa nitakuwa balozi wa kutangaza kiwanda na dawa hizo kwa kila halmashauri atakayopita ili kutoa msukumo wa kununulika bidhaa hiyo.
Nae kaimu meneja mkuu wa Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited, Samwel Mziray  alisema,kwa sasa wanazalisha dawa za aina mbili ambazo ni Bactivec na Griselesf zinazotumika kwa kunyunyuzia katika mazalia ya mbu.
Alifafanua pia wanazalisha kwa wingi dawa hizo ambapo alitaja moja ya nchi iliyonunua dawa hizo ni Niger ambayo tayari imenunua zaidi ya lita 91,000 na nchi nyingine za Serbia na Srilanka ziko katika mazungumzo ya kununua dawa hizo.
“Nikuombe kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,kutoa ujumbe wa kutangaza dawa hiyo kwa halmashauri ambazo bado hazijanunua dawa hizi kukitumia kiwanda hiki kufikia malengo ya Rais dk ,John Magufuli”, alisema Mziray.
Mziray alisema kwa wiki wanazalisha lita 42,000 na zina uwezo mkubwa wa kuangamiza viluwiluwi vya mbu wa malaria.
Kuhusu agizo la Serikali la kuzitaka halmashauri nchini kununua dawa hizo tayari utekelezaji huo umefanywa na wilaya ya Kibaha kupitia ofisi ya mganga mkuu Mkoa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji kwa kufanya majaribio kwenye kata mbili za Mkuza na Visiga na wamejiridhisha .
Kaimu meneja masoko na mauzo kiwandani hapo, Frank Mzindakaya alieleza, serikali inapaswa kutenga bajeti ya kutosha ili kuziwezesha halmashauri kununua dawa hizo.
Alisema, dawa za kiwanda hicho wanaziweka katika vipimo mbalimbali ikiwemo vya lita 20 na ujazo wa miligramu 30 .
Mziray aliwaomba dawa hiyo itumike kwani ikimwagwa katika madimbwi makubwa huua mbu wrote na hatimae kuwalinda wananchi dhidi ya malaria”, alisema Mzindakaya.
    Akielezea juu ya kiwanda hicho ,Mzindakaya alifafanua ,kuwa Tanzania Biotech Products Limited  ni Kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo (NDC) iliyopewa dhamana ya kusimamia na kuendesha kiwanda cha kuzalisha bidhaa hizo. 
         June 6 mwaka huu,mwenge wa Uhuru umepokelewa wilayani Kibaha ,kutoka Kisarawe ,ambapo ukiwa Kibaha ulitembelea miradi 10 yenye thamani ya sh .bilioni 13.775.965 .
       Awali akikabidhi mwenge huo ,mkuu wa wilaya ya Kisarawe ,Happiness Seneda ,alisema June 5 ,mwenge wa Uhuru ,ulitembelea miradi saba iliyogharimu bilioni 3.1 .

No comments