Header Ads

Responsive Ads Here

Ajishindia pikipiki ya Boxer kupitia kampeni ya “Hamasika na Masika “ ya Mobisol


MOBS2
Mwakilishi wa Kampuni wa umeme jua ya Mobisol mkoa wa Dar es Salaam,Allan Rwechungura,akibofya kitufe cha komputa  wakati wa droo ya mwisho ya promosheni ya Hamasika na Masika ambapo mkazi wa kijiji cha Iyale mkoani Mbeya, Baraka Mbale aliibuka mshindi wa pikipiki ya aina ya Boxer wakati wa droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemedy.

MOBS3
Mwakilishi wa Kampuni ya umeme jua ya Mobisol mkoa wa Dar es Salaam, Allan Rwechungura akimpigia mshindi wa Droo ya mwisho ya promosheni ya “Hamasika na Masika” wakati wa droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa kijiji cha Iyale mkoani Mbeya, Baraka Mbale, aliibuka mshindi wa pikipiki ya aina ya Boxer wakati wa droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemed.
………………………………………………………
-Mobisol yafikisha wateja 60,000
Droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Hamasika na Masika”iliyokuwa inaendeshwa na kampuni ya kijerumani ya  kuunganisha na kuuza vifaa vya nishati inayotokana na nishati ya jua ya Mobisol yenye makao yake nchini mjini Arusha imefanyika  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo,Bw.Baraka Mbale kutoka mkoani Mbeya amejishindia zawadi  kubwa ya promosheni ya  Pikipiki mpya ya Boxer.
 
Promosheni hiyo ya “Hamasika na Masika’ ilianza mwezi Aprili na kumalizika leo tarehe moja Juni ambapo ililenga  kuwapa nafasi za kushinda zawadi mbalimbali wateja wapya wa Mobisol pamoja na wateja wa zamani ambao wamewashawishi wateja kununua mitambo bora ya Mobisol. Katika  droo zilizofanyika awali jumla ya washindi sita waliweza kupatikana katika droo mbili za mwanzo, ambapo walijishindia zawadi mbalimbali kama Redio ya Sola, Mashine za kunyolea nywele, pamoja na pesa taslimu.
 
Kampeni hii imekuwa na hamasa kubwa kwa wananchi ambapo taarifa za droo za mwanzoni zilizofanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha zinaonyesha kuwa zaidi ya wateja 3000 wameshiriki.
 
Bw.Baraka Mbale akiongea kwa furaha baada ya kupigiwa simu kuwa amejishindia pikipiki mpya alisema“Kwa kweli siamini macho yangu kama nimeshinda zawadi kubwa hivyo, maana ni sawa na nimepewa mtambo wa Mobisol bure kabisa. Ninayo furaha sana leo, na naamini hii itakuwa chachu hata majirani zangu kununua mtambo wa Mobisol”
 
Mwakilishi wa Mobisol  mkoani wa  Dar e salaam,ndugu Allan Rwechungura amesema kuwa ushiriki  huo wa wananchi wengi unadhihirisha  ni kwa jinsi wanaiamini kampuni ya Mobisol ambayo imejikita katika utoaji wa mitambo ya sola kwa malipo ya pesa taslimu, ama kwa mkopo hadi wa miaka mitatu.
 
 “Nawashukuru sana  wateja wote wa Mobisol ambao wanaendelea kuifanya kuwa kampuni bora zaidi ya sola Afrika Mashariki. Mobisol tunazidi kuwahakikishia kuwa bidhaa zetu ni bora zaidi na kuna bidhaa mpya zinazidi kutolewa kila siku kuweza kumlenga kila mwananchi wa Tanzania na tunafurahi kuona wiki hii tumefikisha wateja 60,000 katika  familia ya Mobisol”Alisema.
 
Alisema kuwa Mobisol inaendelea kuboresha huduma zake nchini kwa kupanua mtandao wake wa kuwaunganisha wananchi na nishati ya jua ikiwemo kuhakikisha wateja wanafurahia matumizi ya nishati hiyo sambamba na watumuaji wa umeme wa kawaida kutokana na kusambaza pia vifaa bora na imara kwa matumizi ya nyumbani na biashara kama vile Redio, Mashine za kunyoa, MobiChaja, tochi pamoja na TV
 
Rwechungura alisema kuwa mwaka huu Mobisol imepania kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya nishati ya Jua, kwa maana hadi sasa tunamuwezesha mteja wetu apate karibu mahitaji yote ambayo angeyapata akiwa na Umeme wa kawaida. Hatutoi tu sola, bali na vifaa karibu vyote ambavyo ni muhimu kwa mahitaji ya nyumbani na biashara kama Redio, Mashine za kunyoa, MobiChaja, tochi pamoja na TV.
 
Alimalizia kwa kuwakumbusha wateja wote wa Mobisol kuwa kila mteja anayeshawishi mteja mpya kujiunga na mtandao huo anafaidika kwa kujipatia kamisheni nono.

No comments