Header Ads

Responsive Ads Here

YANGA YAIPIGA KIPIGO CHA BAO TANO TIMU YA BUSERE SERE FC ,YAHAIDI KUWAPA FURAHA MASHABIKI WAKE ZIDI YA PRISONSDSC_0117
 Timu ya Yanga ikiweka Gori la kwanza ambalo limefungwa na Deus Kaseke aliyefungua pazia hilo la mabao kufunga dakika ya 45 kipindi cha Kwanza.

Mashambulizi yakiendelea kwa Timu zote mbili Yanga na Buseresere FC.YANGA imepoza machungu ya kuvuliwa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayojulikana kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kuwafunga wenyeji, Buseresere mabao 5-0 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Shule ya msingi Waja, Geita.

Yanga Jumapili ilivuliwa ubingwa wa ASFC baada ya kufungwa 1-0 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Na katika kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga walirudi Geita walikopita kabla ya kucheza na Mbao, kucheza mchezo wa kirafiki.  


Na wakawaonyesha mashabiki wao kwamba kipigo cha Mbao ilikuwa ni kuteleza tu, kwani wao bado imara kabisa – baada ya kuitandika Buseresere 5-0. 


Mabao ya Yanga leo yamefungwa na viungo Emmanuel Martin mawili dakika za 49 na 72, Deus Kaseke dakika ya 44 na washambuliaji Matheo Anthony dakika ya 88 na Amissi Tambwe dakika ya 90.


Pamoja na kufungwa, mabingwa wa mkoa Geita, Buseresere walionyesha upinzani kwa mabingwa wan chi Yanga.


Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Benno Kakolanya/Ally Mustafa ‘Barthez’ dk78, Juma Abdul/Hassan Kessy dk77, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan/Nadiri Haroub ‘Cannavaro’ dk78, Saidi Juma ‘Makapu’/Thabani Kamusoko dk85, Deus Kaseke/Simin Msuva dk75, Justin Zulu, Juma Mahadhi/Amissi Tambwe dk75, Matheo Anthony na Emmanuel Martin/Geoffrey Mwashiuya dk75. 


Yanga inatarajiwa kuondoka Geita Alhamisi kurejea Dar es Sakaam tayari kwa mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Prisons Uwanja wa Taifa Jumamosi.  


IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

No comments