Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI PROFESA MBARAWA KUMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KIGALI, RWANDA


pic+mbarawa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameondoka nchini leo kwenda Kigali Rwanda, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye mkutano wa siku mbili wa “Transform Africa Summit 2017”.

Mkutano huo utawakutanisha viongozi na wataalam mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kujadili masuala kadhaa ikiwemo maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), hususan katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika mkutano huo, Profesa Mbarawa ataeleza kwa kina changamoto na mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania katika uwekezaji wa Miundombinu ya Habari na Mawasiliano, Maendeleo ya Sera na Miongozo inayotumika hapa nchini katika kusimamia sekta hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuiunganisha Tanzania na Mataifa mengine.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
10 Mei, 2017

No comments