Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI MAGEMBE APIGA MARUFUKU UPIGAJI MINADA YA NG’OMBE KWENYE HIFADHI.


1488617830-maghembenew
Na Tiganya Vincent, Kahama May 29, 2017

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa  Jumanne Maghembe amepiga marufuku minada ya ng’ombe zinazokamatwa katika Mistu ya Hifadhi kufanyika katika maeneo hayo  badala yake ifanyike katika maeneo ya wazi ili kutoa  nafasi kwa wananchi kushiriki kwa uwazi.

Waziri Magembe alisema hayo juzi mjini Kahama katika ziara yake wilayani kahama kufuatia oparesheni za kuondoka mifugo kwenye Mistu ya Hifadhi ambapo mifugo hiyo imekuwa ikipigwa mnada ndani ya hifadhi badala ya maeneo ya wazi.

Kwa mujibu wa waziri Magembe utaratibu huo wa kuendesha minada ndani ya Mistu ya Hifadhi umekuwa ukiwanyima nafasi wananchi pamoja na wamiliki wa mifugo hiyo kushiriki katika zoezi hilo.

Alisema kuwa wakati utaratibu huo umewafanya baadhi Maafisa waliohusika na ukamataji wa mifugo katika eneo hilo wajihusishe na ununuzi wa ng’ombe hizo na hivyo kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi na kushindwa kutenda haki kwa watu wote hata wale ambao mifugo yao imekamatwa.

Profesa Maghembe alisema kuwa kabla ya mnada haujafanyika ni vema Mkuu wa Wilaya husika afahamishwe ili yeye na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama iwepo wakati wa uendeshaji wa zoezi hilo ili kuondoa manung’uniko kutoka kwa wenye mifugo na wananchi.

Waziri huyo aliongeza kuwa ni vema kabla ya siku ya mnada kufanyika , Mkurugenzi Mtendaji akataarifiwa ili awatangazie wananchi wote katika eneo lake kwa ajili ya kushiriki mnada hatua itakayoondoa malalamiko.

Naye Meneja wa Pori la Akiba la Moyowosi Kigosi Patrick Kutondolana alisema kuwa hifadhi hiyo inakabiliwa na tatizo kuwepo kwa kundi kubwa la ng’ombe kutoka nchi za jirani ambazo zimekuwa zikichungwa katika eneo hilo na ndipo ndani yake majangili utumia mwanya huo kuwinda wanyamapori kinyume cha sheria.

Alisema kuwa tatizo jingine ni kwa wale watu wanaopewa vibali vya kulina asali badala yake wamekuwa wakitumia vibali hivyo kuendesha shughuli za ujangili  na kuwinda wanyama mbalimbali huku silaha zao wakiwa wakificha katika mizinga ya asali.

Meneja huyo aliongeza kuwa wakimbizi kutoka Kambi ya Nduta mkoani Kigoma wamekuwa wakiingia katika Hifadhi hiyo na kuendesha shughuli za ujangili kwa kutumia silaha za kivita ambazo wametoka nazo makao kisha kurudi makambini.

Waziri Maghembe alikuwa na ziara katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera kwa ajili ya kuangalia zoezi la uondoaji wa watu waliovamia katika maeneo mbalimbali ya Hifadhi.

No comments