Header Ads

Responsive Ads Here

WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS


unnamed
Mkuu wa Kitengo cha Maabara ya Uhandisi  Ujenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Stephen Minja akionesha kwa waandishi wa habari vigae vilivyofikishwa katika maabara hiyo ili kudhibitishwa ubora wake.

A
Mkuu wa Kitengo cha Maabara ya Uhandisi  Ujenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Stephen Minja akionesha kipande cha Bomba kilichohakikiwa ubora katika maabara hiyo.
A 1
Mkuu wa Kitengo cha Maabara ya Uhandisi  Ujenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Stephen Minja akionesha kwa waandishi wa habari lami iliyofikishwa katika maabara hiyo ili kudhibitishwa ubora wake kwa mujibu wa sheria ili iweze kutumika katika ujenzi wa barabara hapa nchini.
A 2
 Mkuu wa Kitengo cha Maabara ya Uhandisi  Ujenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Stephen Minja akipima ubora wa Lami kwa kutumia mashine maalum ili kudhibitisha kama ina ubora unaotakiwa kulingana na viwango vilivyowekwa.
A 3
Mtaalamu wa masuala ya Umeme kutoka shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw. Evance Jeremiah akionesha namna mitambo ya kupima ubora wa vifaa vya umeme inavyofanya kazi.A
(Picha na Maelezo).
……………………….
Frank Mvungi -MAELEZO
DAR ES SALAAM
SERIKALI  imewataka wazalishaji na wajasiriamali  nchini kuhakikisha kuwa bidhaa wanazozalisha zinakidhi viwango vya ubora vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuchochea ukuaji wa uchumi.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Maabara ya Uhandisi wa  Ujenzi ya Shirika la Viwango Nchini,  Mhandisi Stephen Minja wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea na kujionea namna maabara za shirika hilo zinavyotekeleza jukumu lake la kuhakiki viwango vya ubora hapa nchini.
Akifafanua zaidi Minja amesema kuwa mabara za shirika hilo zipo kwa ajili ya kuhudumia wazalishaji wa bidhaa mbalimbali na wale wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi  lengo ili kuhakiki ubora wa bidhaa zote ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza kwa watumiaji.
“Maabara yetu ina viwango vya kimataifa na gharama zake ni nafuu ambazo kila mwananchi anaweza kumudu lengo likiwa ni kutoa huduma kwa wananchi na kuchangia kuchochea maendeleo  kwa kudhibiti bidhaa hafifu” alisema  Minja
Aliongeza kuwa maabara hiyo inapima bidhaa za ujenzi kama  nondo, chokaa, vigae, mbao, mabomba ya maji, simenti, nguzo za umeme,matofali,zege, mchanga na bidhaa zote zinazotumika katika ujenzi wa barabara ikiwemo lami.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa kitengo cha maabara ya umeme,  Mhandisi Anectus Ndunguru amesema kuwa vifaa vyote vya umeme vinavyozalishwa na kuingizwa nchini lazima vipimwe ubora wake kuona kama vinakidhi vigezo ili kuepusha majanga.
Alitaja baadhi ya vifaa ambavyo lazima vihakikiwe ubora wake kuwa ni vifaa vyote vinavyotumika katika kujenga mfumo wa umeme katika majengo, taa za majumbani, pasi, redio, televisheni, waya .
Akizungumzia athari za kutumia vifaa visvyo na ubora Ndunguru amesema kuwa athari za matumizi ya vifaa hivyo ni makubwa ikiwemo kusababisha majanga na kupotea kwa umeme hivyo kuongeza gharama kwa mtumiaji.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekuwa likisisitiza matumizi ya bidhaa zenye ubora na zilizohakikiwa na kuepuka bidhaa hafifu ambazo kwa sasa zimedhibitiwa na shirika hilo kwa kiwango kikubwa hali inayochochea ukuaji wa sekta ya Viwanda hapa nchini.

No comments