Header Ads

Responsive Ads Here

WATU WAWILI WAMEUWAWA MMOJA KATIKA AJALI NA WAPILI KUPIGWA HADI KUFA WILAYANI KONDOA


KONDOA
Na Mahmoud Ahmad, Kondoa

Watu wawili ambao hawajatambuliwa majina yao hadi sasa wanaokiwa kuwa
na umri tofauti kati ya miaka 37 hadi 40 mmoja dereva wa Katapila
lenye no za usajili T 370 BBG lililokuwa likitengeneza barabara ya
Haubi na kumgonga mtu mmoja hadi kufa na wananchi wenye hasira kumpiga
dereva huyo hadi kumuua.

Tukio hilo limetokea wilayani Kondoa DC Kata ya Haubi kijiji cha haubi
baada ya dereva huyo ambaye jina lake halijapatikana hadi sasa
kumgonga mwenda kwa miguu na kusababisha kifo chake hapo hapo.
Mmoja wa mashuhuda aliekuwepo eneo la tukio Mohammed Kijaji alisema
kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 12;45 jioni ya tarehe 13 mwezi
huu baada ya mwenda kwa miguu huyo ambaye hakutambuliwa jina kuwa
anatembea pembezoni mwa barabara na ndipo katapila hilo kumgonga na
kufa hapo hapo.
Kijaji alisema kuwa wananchi wenye hasira kali ndipo walimvamia
mwananchi huyo na kumpiga hadi kufa dereva huyo na kusababisha mauti
yake papo hapo na baada ya kumuuwa waliendelea kuleta fujo hadi polisi
walipofika eneo la tukio na wananchi hao kutawanyika.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo la kuuwawa kwa watu wawili mmoja kwa ajali na
mwingine kwa kupigwa na wananchi hadi kufa na jeshi la polisi
linawashikilia watu wawili kwa mauuaji ya dereva huyo
Kamanda Mambosasa akizungumza kwa njia ya simu alitoa wito kwa
wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi na jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ambapo maiti za marehemu hao
zikihifadhiwa chumba cha maiti hospitali ya wilaya ya Kondoa.

No comments