Header Ads

Responsive Ads Here

WASICHANA 82 KATI YA 276 WA SHULE YA CHIBOK, WAACHIWA HURU NA BOKO HARAM


Wasichana walioshikwa mateka wakipanda helikopta ya jeshi


NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari

WASICHANA 82, waliotekwa  nyara na kundi la Boko Haram nchini Nigeria wakiwa bwenini kwenye shule moja ya Chibok nchini humo, kiasi cha miaka mitatu iliyopita, wameachiwa huru Mei 7, 2017.

Wasichana hao wameachiwa kwa kubadilishana na viongozi watano wa Boko Haram na ni matokeo ya majadiliano ya miezi kadhaa yaliyohusisha wapatanishi toka mabara mawili.

Hata hivyo, wasichana hao ambao wakati wanachukuliwa mateka walikuwa ni wanafunzi, wameacha wenzao kadhaa bado wakishikiliwa. Boko Haram iliwachukua mateka jumla ya wasichana wa shule 276 wakiwa kwenye mabweni ya shule mnamo Aprili,  2014.

Kuachiwa huru kwa wasichana hao, kuna fuatia 
majadiliano yaliyoratibiwa na Mustapha Zanna ambaye anaendesha kituo cha yatima huko Maiduguri ambaye awali alikuwa mwanasheria wa mwasisi wa kundi hilo la Boko Haram, Mohammed Yusuf, lakini pia majadiliano hayo yaklihusisha serikali ya Uswis na Msalaba Mwekundu.

Wakiwa kwenye pick-up ya Msalaba Mwekundu, na wakiwa wamevalia T-shirts zenye nembo ya Msalaba Mwekundu, walionekana wakipanda helikopta ya jeshi na kusafirishwa kwenda mji mkuu Lagos kukutana na Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari

No comments