Header Ads

Responsive Ads Here

WALIMU, WATU WAZIMA WATAKAOWAPA UJAUZITO WANAFUNZI KUKIONA CHA MOTO


bue1
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhozya baada ya kukagua ujenzi wa vyoo.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Frank Bahati, kushoto ni Katbu Tawala mkoa huo Kamishna wa wa Polisi Cloundwing Mtweve na nyuma ya mkuu wa mkoa ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Deo Alpnhonce.

bue2
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akimwuliza jambo  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi na Ufundi Bukongo, Lea Kalua wakati akikagua utengenezaji wa madawati shuleni hapo juzi.
bue3
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akisisitiza jambo mara baada ya kukagua utengenezaji wa madawati wa juzi , kshoto ni Katibu Tawala Kamishna wa Polisi Cloundwing Mtweve, wa pili  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi na Ufundi Bukongo, Lea Kalua , Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estiah Chang’a wa kutoka kulia na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Frank Bahati kulia .
bue4
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akihutubia mkutano wa hadhara mjini Nansio baada ya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo wilayani Ukerewe.
bue5
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akikagua ujenzi wa vyoo katika Shule ya Msingi Muhozya juzi ambapo pia alikagua na kushiriki  ujenzi kama huo katika Shule ya Msingi Chabilungo na kuchangia mabati 32 yenye thamani ya shilingi 500000 .Pia aliendesha harambee ya papo hapo na kupata sh 300000 naye akicangia sh. 100000.
Picha zote na Baltazar Mashaka
……………………………………………………………………………………
NA BALTAZAR MASHAKA, UKEREWE

WALIMU  na Watu wazima watakaobainika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi kisha kuwapa ujauzito watakumbana na mkono wa sheria bila kuonewa haya wala huruma.

Kauli hiyo ilitolewa juzi wilayani Ukerewe na Mkuu wa Mkoa wa Mwaza John Mongella wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu wilayani humu.

Alionya kuwa ni marufuku kuunda tume ya kuwachunguza watuhumiwa walimu wenye matatizo ya aina hiyo kwa ngazi walizofikia kuwajaza wanafunzi ujauzito.
 
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Frank Bahati alimweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa tangu afike wilayani humo hajawahi kupata taarifa aua kesi za wanafunzi kupewa ujauzito.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa alimwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe (OCD) Ignus Kapira kuwa uchunguzi wa kesi hizo usikuchukue wiki moja.

“ Ni marufuku kuunda tume ya kuchunguza watuhumiwa wa aina hiyo.Tatizo hili la mwalimu kwa ngazi uliyofikia unampa ujauzito mwanafunzi upate nini,
 
“ Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi,  OCD tena wewe tumekuleta hapa ni  mpya kesi hizo za kubaka usimwachie mtu.Kama ni kiongozi,mwalimu ama mtu mzima,usimwachie mtu huyo nenda mahakamani kasimame naye mahakamani kama nako kuna tatizo nipigie simu tuhangaike naye huyo mtu,”alisema.

Mongella alisema kuwa mwalimu au mtu mzima anayekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtoto wa shule (mwanafunzi) haiwezekani na haikubaliki lazima serikali itakufa nao kwa kuwaharibia masomo yao.

No comments