Header Ads

Responsive Ads Here

UVCCM YASHITUKIA MCHEZO MCHAFU KISIASA


mpanda3
Na Mwandishi wetu, Rukwa

Umoja wa Vijana wa CCM umewaonya watendaji wake
kujiepusha na uvunjaji wa kanuni na maadili ya jumuiya  hiyo ikiwemo
kuendesha mijadala inayozmgumzia masuala ambayo yaliopitishwa kwa mujibu
wa vikao,  kikanuni na katiba ya CCM.

Pia umoja huo umelaani na kusema kitendo chochote  cha
utovu wa nidhamu na ukiukaji maadili kitakachothibitika kufanywa na
mtendaji husika katika ngazi ya jumuiya hatua za kimaadili na kikanuni
zitafuata haraka sana.
 

Msimamo huo umetolewa  na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM
Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na watendaji
wa jumuiya hiyo ngazi za matawi, kata na wilaya na mkoa katika mkoa wa
Katavi na Rukwa.  
 

Shaka alisema jumuiya ina taarifa za kutosha kwamba kuna
baadhi ya watendaji wanatumiwa na maadui ili kutaka kudhoofsha juhudi
na mikakati ya umoja huo kwa njia za mitandao ya kijamii na magazeti. 

Alisema UVCCM itatumia njia na vyanzo vyake muhimu  kupata ushahidi kamili dhidi ya wanaoshiriki  uhalifu huo na kuchukua hatua stahiki za kinidhamu na kanuni  dhidi ya watendaji hao ikiwemo  kutaja majina yao na wanaoshirikiana nao .

“Zipo juhudi na mikakati batili ambayo naamini haitafua dafu ya kutaka kuichafua jumuiya yetu kwa maneno ya uzushi na upotoshaji, inashangaza  kusikia baadhi ya watendaji wetu nao
wanashiriki kucheza ngoma hiyo ya wachawi wa CCM na jumuiya zake
tunajuwa na tunatafahamu yako makoloni ya watu bado yamo ndani
tumeshakula kiapo tutambana nao na tunawahakikishia CCM iatabaki salama
hawatafanikiwa nia zao ovu “Alisema Shaka akionekana kukerwa. 

Aliwaeleza watendaji hao kwamba kila uamuzi unaofanyika
ndani ya chama na jumuiya zake ni maamuzi yanayopitishwa kikanuni na
kikatiba bila kukiukwa utaratibu au miongozo husika.  

Aidha shaka aliwakanya watendaji na wana jumuiya ambao
wanadhani hoja zao zinaweza kuwa na mashiko au nguvu kuliko matakwa na
mashari ya msingi  yatokanayo na kanuni na katiba ya CCM .

“Nmekuwa nikipigiwa simu nyingi na baadhi ya waandishi
wakidai kuna watendaji wa uvccm wanapigana uteuzi wa Nafasi fulani
wengine wakienda kudai madai kwenye vyombo vya habari hivi 

unapingaje maamuzi ya kikanuni na kikatiba, anayepinga
maamuzi hayo anatumwa kwa nguvu za kishetani na unakwendaje kudai madai
ya uhamisho kupitia vyombo vya habari sio maadili ya uongozi wa chama
chetu chama hiki kinautaratibu mzuri sana wa
kushuhulikia mambo yake ya ndani kuanzia kata shina hadi taifa:Akieleza
 

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema wapo watu ambao awali
walidhani  jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM  isingekuja juu na
kusimamia misingi yake hivyo wanapona kuna ishara njema za mafanikio
wameamua kuanza kutunga na kuzusha mambo ya yasiyo ya msingi.

“Wana jumuiya wahoji masuala ya msingi yanayohusu uhai
na maendeleo ya uvccm ni haki yao lakini watumie  vikao halali vya
kikanuni na kikatiba kuelezea hoja zao na madai yao ikiwa ya ufisadi au
wizi huku wakionyesha ushahidi, kulalamika mitandaoni
na magazetini hakuleti ufumbuzi wala hawakisaidi chama na jumuiya na
sio utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi chama chetu ni kikubwa kina maadili
na miongozo yake hatuwezi kuvumilia vitendo vya utovu wa nidhamu na
ukosefu wa maadili ya uongozi” Alisistiza kaimu
huyo Katibu Mkuu. 
 

Shaka amekamilisha ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na
jumuiya zake katika mikoa Katavi na Rukwa na kesho (Leo) anatarajiwa
kuanza ziara ya kikazi katika mikoa ya Pwani na Dar es Saalam kutembelea
wilaya zote za mikoa hiyo.

No comments