Header Ads

Responsive Ads Here

USIRI NI MOJA YA CHANGAMOTO KUBWA KATIKA KUSHUGHULIKIA KESI ZA WAATHIRIKA WA UKIMWI.


Habari/ Picha na Philemon Solomon.
……………………
Usiri ni moja ya changamoto kubwa katika kushughulikia kesi za waathirika wa ukimwi walioambukiza kwa makusudi tangu sheria ya kudhibiti watu wanaoambukiza ukimwi kwa makusudi mwaka 2008 nchini. 
1
Mkuu wa kitengo cha sheria kutoka Tume ya kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS), Elizabeth Kaganda.
Akizungumza mjini Dodoma wakati wa  semina ya wahariri wa vyombo vya habari pamoja na kamati ya kudumu ya bunge ya kudhibiti Ukimwi iliyokuwa ikijadili utekelezaji wa sheria ya ukimwi na haki za Binadamu, mkuu wa kitengo cha sheria kutoka Tume ya kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS), Elizabeth Kaganda amesema kwamba kifungu cha 47, cha sheria ya ukimwi namba 28 ya mwaka 2008, kwamba mtu aliyeambukizwa ukimwi kwa makusudi anapaswa kutoa ushahidi na ushirikiano kwa Jamhuri ili kuweza kufanikisha kesi hizo.
” tatizo linakuwa baada ya wale walioambukizwa kuwa ni watu wazima na hawapo tayari kutoa siri ya matatizo yaliyowakuta ( right to privacy) usiri ndio changamoto kubwa kwa watu wazima kwa kuwa wengi  hawapo tayari kuweka mambo yao ya siri hadharani ” amesema kaganda, 
2
Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile ambaye pia  Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya masuala ya Ukimwi akizungumza wakati wa semina.
Pia Wabunge wa kamati ya kudumu ya ukimwi wameitaka serikali kuja na  uchambuzi wa sheria ya maambukizi ukimwi, akizungumza na waandishi wa habari , Mbunge wa kigamboni, dk faustine ndugulile amesema kwamba wabunge wanataka kujua kupitia sheria ya kudhibiti ukimwi ni watu wangapi wametiwa hatiani kwa kosa la kuambukiza wenzao kwa makusudi.
Alisisitiza kwamba pia wabunge wameonyesha wasiwasi kwa sababu unapopima mtu afya yake ni siri yake  kwahiyo ni ngumu kumuweka hadharani  lakini hapo wana jukumu LA kulinda jamii.
Amesema wabunge walikuwa kwenye semina kupitia kamati yao ya ukimwi na madawa ya kulevya katika juhudi za kuendelea kupambana na janga hilo katika jamii.
Kuna udhaifu Mkubwa katika sheria ya kuzuia maambukizi ya ukimwi ya makusudi. 
3
Naibu waziri wa kazi, ajira, vijana na walemavu, Anthony Mavunde. 
Naibu waziri wa kazi, ajira, vijana na walemavu, Anthony Mavunde amesema kwamba serikali itakwenda kubadilisha sheria ili kupunguza udhaifu na mapungufu katika kuendelea kuzuia maambukizi ya ukimwi kwa makusudi ndani ya jamii.
“serikali imepokea maoni ya wabunge juu ya mapungufu ya sheria ya maambukizo ya ukimwi kwa makusudi na inakwenda kuifanya kazi ili kuendelea kuilinda jamii kwa kuiangalia upya hayo mapungufu, ” amesema mavunde
Kamati ya kudumu ya bunge ya ukimwi na madawa ya kulevya na wahariri wa vyombo vya habari watakaa pamoja ili kujadili hali ya maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini pamoja na sheria ya mwaka 2008 na changamoto zake
5
 Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Tacaids, Yasin Abbas akitoa mada.
Wabunge wakichangia mada mbalimbali wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari pamoja na kamati ya kudumu ya bunge ya kudibiti Ukimwi iliyokuwa ikijadili utekelezaji wa sheria ya ukimwi na haki za Binadamu.
6
7
8
Wabunge wakichangia mada mbalimbali wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari pamoja na kamati ya kudumu ya bunge ya kudibiti Ukimwi iliyokuwa ikijadili utekelezaji wa sheria ya ukimwi na haki za Binadamu.

No comments