Header Ads

Responsive Ads Here

UONGOZI WA YANGA WAKATAA OMBI LA MANJI


Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wao Yusuf Manji alieamua kujiweka pembeni ndani ya klabu hiyo baada ya kuiongoza kwa kipindi cha miaka 11.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Siza Lymo alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi bado wanashindwa kulitolea ufafanuzi zaidi kwani kwao wamepatwa na taharuki juu ya jambo hilo.

Alisema kwamba kwa upande wao bado hawajaridhia jambo hilo na kama kamati ya utendaji wapo katika mkakati wa kwenda kwa mwenyekiti kumuomba ili abatilishe uwamuzi wake.

Aidha kwa upande mwingine kiongozi wa matawi ya klabu ya Yanga Bakili Makele alisema kwamba hapo kesho wanataraji kuwa na kikao cha viongozi wa matawi ili kulijadili swala hilo kwa undani zaidi.

Makele alisema kwamba licha ya kuandika barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kukaa kimya kwani bado wanamuhitaji Manji na watafanya jitihada kubwa ili aendelee na majukumu ya klabu.

No comments