Header Ads

Responsive Ads Here

TIMU YA VIONGOZI WA SERIKALI MBEYA YAIBAMIZA TIMU YA VIONGOZI WA DINI MABAO 4 KWA 1


Timu ya VIONGOZI wa serikali chini ya uongozi wa kocha mchezaji Mkuu wa Mkoa wa Mbeya imeibamiza bila huruma timu ya VIONGOZI wa DINI mabao 4-1 Mpira ulikuwa mkali  ila timu ya VIONGOZI wa serikali iilionekana kucheza kwa maelewano hivyo kuisaidia timu hiyo kuibuka mshindi na kumaliza tambo za muda mrefu za timu hizo angalia matukio katika picha hapa chini
AMO1
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akikokota mpira mbele ya mchezaji wa timu ya viongozi wa dini katika mchezo uliofanyika leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku viongozi  Timu ya viongozi wa Serikali ikitoka kifua mbele kwa kushinda magoli 4-1 dhidi ya timu ya viongozi wa dini.

AMO2
Wachezaji wa timu za viongozi wa Dini na Viongozi wa Serikali zikichuana vikali kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika leo.
AMO3
Mchezaji wa timu ya Viongozi Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akinyanyua juu kombe waliloshinda dhidi ya timu ya viongozi wa Dini katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.
AMO4
Mchezaji wa timu ya viongozi wa serikali na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kwye uwanja wa Sokoine ambapo timu yake imeifunga timu ay viongozi wa dini magoli 4-1.
AMO5
Wachezaji wa timu ya viongozi wa serikali wakipiga picha ya pamoja na kombe lao mara baada ya ushindi huo.
AMO6
Timu ya viongozi wa dini ikikaguliwa na mgeni rasmi kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

No comments