Header Ads

Responsive Ads Here

TGNP MTANDAO YAWAPONGEZA WASICHANA WALIOFANYA VIZURI KATIKA VYUO VIKUU NCHINI

 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi (katikati), akizungumza na waandishi habari wakati wa  kuwapongeza wahitimu waliofanya vizuri katika vyuombalimbali nchini katika ukumbi wa TGNP  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhitimu Joan Zenas na Flora Njiku mhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kairuki.


Mhitimu,  Joan Zenas akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Taswira ya ukumbi wakati wa mkutano huo.
Wanafunzi hao wakiwa kwenye majadiliano.
Ofisa Ujenzi wa Nguvu ya Pamoja wa TGNP Mtandao, Anna Sangai akizungumza na wanafunzi hao.
Mkufunzi Petra Letter kutoka kutoka Chuo cha GTT akichangia mada.

Na Mwandishi Wetu

TGNP Mtandao imesema kuwa changamoto inayowakabili wanafunzi wa vyuo  vikuu nchini ni rushwa ya ngono.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wasichana 38  waliofanya vizuri katika elimu ya Juu kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa  TGNP,  Lilian Liundi amesema wanawake wengi wanashindwa kufikia malengo kutokana na changamoto ya ngono na kufanya wanawake kuwa wanyonge.

Amesema kuwa wanawake wanaonekana daraja la pili hali ambayo inafanya kuendelea kuweka mfumo dume wa maamuzi kufanywa na wanaume.

Lilian amesema kuwa wasichana ambao wamefanya vizuri  katika vyuo mbalimbali inaonyesha ukombozi wa wanawake katika kuleta maendeleo ya kumuokoa mwanamke mwezie.

Aidha amesema kuwa TGNP Mtandao imekuwa katika mstari wa mbele katika kuendesha harakati za kumkomboa mwanamke katika changamoto mbalimbali.

Mmoja wahitimu wa waliofanya vizuri , Aisha Soudy  kutoka  Chuo cha  Teku, amesema kuwa wasichana wanachangamoto nyingi ikiwemo na mila na tamaduni ambayo unampendelea zaidi mtoto wa kiume.

Amesema kuwa yuko tayari katika kufanya ukombozi wa mwanamke kwa kutoa msaada pale anapoona anawajibu wa kufanya kwa ajili ya kumuinua Mwanamke.

Kwa upande wa Mhitimu aliyefanya vizuri katika matokeo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela amesema kuwa msichana ana nafasi yake kama  akijitambua anataka kufanya nini katika jamii yake katika kuleta tofauti  kuliko vile wanavyofikiria.
Sara amesema kuwa licha kukabiliwa na changamoto kama mtoto wa kike lakini ameweza kufanya vizuri na kuwataka wasichana kujiamini kuwa wanaweza.

No comments