Header Ads

Responsive Ads Here

TBL Group kuendelea kuunga mkono mpango wa ‘Mwanamke wa wakati Ujao’


NDAL1
Mmmoja wa wahitimu wa mafunzo ya mpango wa Mwanamke wa wakati Ujao  ,Warda Kimaro kutoka TBL Group,akipokea cheti kutoka kwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako wakati wa mahafali yaliyofanyika  katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam ,kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri nchini,Mh.Almas Maige.
NDAL2
Mmoja wa wahitimu kutoka TBL Group,Neema Arora akipokea cheti baada ya kuhitimu na kufaulu mafunzo ya kozi hiyo
NDAL3
Meneja wa ukuzaji vipaji wa TBL Group,Lilian Makau Galinoma akitoa mada wakati wa hafla hiyo ya mahafali ya kozi ya Mwanamke wa Wakati Ujao
NDAL4
Warda na Neema wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea vyeti vyao
NDAL5
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo haya katika picha ya pamoja
NDAL6
Wahitimu kutoka TBL Group (walioshika vyeti) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzao walioungana nao katika mahafali iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
……………………………………………………………………………………..
-Kuzidi kutoa fursa sawa za uongozi ndani ya kampuni
Kampuni ya TBL Group imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jithada za kuwajengea uwezo wafanyakazi wake wanawake kwa kuwawezesha kushiriki mafunzo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya mpango wa ‘Mwanamke wa wakati ujao’ yanayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na taasisi ya Confederation of Norwegian Enterprises (NHO)
 Akiongea wakati wa mahafali ya pili ya mafunzo hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa Wiki ,Meneja wa ukuzaji vipaji  wa TBL Group,Lilian Makau Galinoma ,alisema kampuni  itaendelea kuwa mdau wa mafunzo haya kwa kuwa moja ya dhamira yake kupitia mpango wa Women Working  Group ni kuwajengea  uwezo wafanyakazi wake wanawake na kuwapatia fursa za uongozi wa vitengo mbalimbali ambapo wanaendelea kufanya vizuri na kudhihirisha kuwa ujuzi hauna jinsia.Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako.
 “Programu hii ni nzuri hususani kwa wanawake kwa kuwa mafunzo wanayoyapata yanawaongeza uwezo wa kujiamini  na yanaendeshwa zaidi kwa vitendo kuliko nadharia na kuna haja ya kuwa na programu nyingi za aina hii ili ziwafikie wanawake wengi popote walipo nchini”.Alisema.
 Wafanyakazi wa TBL Group ambao ni miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo,Warda Kimaro na Neema Arora walieleza katika mahojiano jayo kuwa  licha ya kwamba wamepitia vyuo vikuu na kupata mafunzo ya kitaaluma lakini mafunzo haya chini ya mpango wa ‘ Mwanamke wa wakati Ujao’yamewawezsha kujua mambo mengi  zaidi na kuwajengea uwezo wa kujiamini katika kutekeleza majukumu yao ya kazi hususani   utawala  na jinsi ya kushiriki na kutoa mawazo kwenye vikao vya bodi.
 “Nashukuru wajiri wangu TBL Group kwa kunipatia fursa ya kushiriki mafunzo haya ambayo yanafanyika kwa vitendo kwa kuwa nimeweza kujua mambo mengi  na  natoa wito kwa wanawake popote  walipo kujiendeleza zaidi kielimu kwa kuwa silaha pekee ya kumkomboa mwanamke ni elimu”Alisema Warda ambaye ni Meneja wa Chapa katika kiwanda cha TDL.
 Kwa upande wake Neema Arora alisema kuwa anatamani zingekuwepo programu kama hizi nyingi hapa nchini kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kupata mafunzo ya nadharia na vitendo kwenye fani mbalimbali ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi ‘Programu hii ni nzuri na imeniwezesha kupata maarifa zaidi hususani katika masuala ya utawala,naishukuru TBL Group kwa kuwa na mkakati wa kuwapatia wanawake fursa za uongozi ndani ya kampuni”.Alisema Neema ambaye ni Mpishi Mkuu wa kiwanda cha Darbrew.
 Akitoa historia ya mafunzo yanayotolewa chini ya mpango huo,Mkurugenzi wa ATE,Dk.Aggrey Mlimuka alisema yanaendeshwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya Confederation of Norwegian Enterprises na hapa nchini yanaendeshwa kwa kushirikiana na chuo cha Eastern and Southern African Management Institute  (ESAMI) kilichopo mkoani Arusha na zaidi ni ya vitendo kuliko nadharia “Wanafunzi wanaojiunga na mafunzo ya mpango huu wanaweza kukutana darasani katika siku 14 ndani ya kipindi cha miezi tisa zaidi ya hapo  wanakuwa wanajisomea na kufanya kazi kwa vitendo katika sehemu zao za kazi na wanapofikia mwisho wa mafunzo wanafanya mitihani na kutunukiwa vyeti kwa wale wanaofaulu”.Alisema.
 Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako, alipongeza wadau wote wanaofanikisha mafunzo haya na alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kuwapatia wanawake nafasi ya kupata mafunzo haya ili yawawezeshe kuwa na uwezo wa kushika nafasi za uongozi wa juu katika sehemu zao za kazi kwa kuwa dunia ya sasa inahitaji elimu ya kisasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuleta ufanisi katika sehemu za kazi

No comments