Header Ads

Responsive Ads Here

TAMASHA LA MUZIKI WA INJILI LENYE UBORA WA KIMATAIFA KUFANYIKA JUMAPILI HII KWENYE UKUMBI WA KANISA LA CITY CHRISTIAN CENTER JIJINI DAR


Tamasha  la muziki wa injili  lenye ubora wa kimataifa  litafanyika Jumapili ya tarehe 21  katika ukumbi wa  Kanisa la City Christian Center (CCC Upanga mkabala na Mzumbe University

Tamasha hili linalojulikana  Ni Salama moyoni, ambapo mwanamuziki Mchungaji PAUL SAFARI  ndiye atakayekuwa muhusika mkuu ambapo atarekodi nyimbo zake kwa njia ya moja kwa moja (yaani live).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Mchungaji SAFARI amesema tamasha hilo limeandiliwa kwa katika viwango  vya ubora wa hali ya juu ili kuendana na viwango vya Kimataifa.
“Ki ukweli tumejiandaa vizuri katika maombi, mazoezi na maandalizi yote ya tamasha. Hili siyo tukio la kukosa maana kila mmoja atae hudhuria ataondoka na furaha na baraka za Mungu”. amesema mchungaji Safari.
Wanamuziki mbali mbali kama a John Lisu, Moses Zamangwa na Movement for Christ nao watatumbuiza katika tamasha hilo linalotarajiwa kuvuta watu wengi.
Mchungaji  Safari Paul ni mmoja wa wachungaji  katika kanisa la DPC na pia mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili. Amekuwa sehemu ya watu waliokuza muziki wa injili Tanzania na amelea na kukuza waimbaji wengi, na ameshiriki kurekodi nyimbo akishirikiana na vikundi mbali mbali ndani na nje ya nchi.
Albamu yake ya kwanza  inayoitwa Furaha ya Bwana mwaka 2006. Na sasa baada ya miaka kumi na moja, Pastor Safari ameandaa Ni Salama Mubashara au Live DVD recording ya Ni Salama.
Tamasha hili la aina yake, limeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu ili kuendana na viwango vya Kimataifa. “Ki ukweli tumejiandaa vizuri katika maombi, mazoezi na maandalizi yote ya tamasha. Hili siyo tukio la kukosa maana kila mmoja atae hudhuria ataondoka na furaha na baraka za Mungu”. asema Pastor Safari. Tamasha hili la Ni Salama yaani Ni Salama Live DVD recording, litafanyika tarehe 21/05/2017 katika Kanisa la City Christian Center (CCC Upanga mkabala na Mzumbe University). Pia Pastor Safari atasindikizwa na John Lisu, Moses Zamangwa na Movement for Christ.
Lengo ni kupeleka ujumbe wa neno la Mungu duniani kote kwa njia ya muziki na uimbaji na kuleta madariko katika maisha ya watu.
 “Watanzania tunasifika sana kwa uimbaji na tumejaliwa na Mungu katika eneo hili, lakini miziki yetu haifiki mbali kwa sababu tunakosa ufanisi na ubora katika kazi zetu. Naami Tamasha la Ni Salama litakuwa ni chachu kwa wanamuziki na waimbaji wote. Narudia tamasha hili litaweka historia. Hivyo usikose” asema Pastor Safari Paul.

No comments