Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOANI MWANZA JANA


msangii-1
TAREHE 25.05.2017 MAJIRA YA SAA 22:15HRS USIKU KATIKA MTAA WA KANYERERE KATA YA MAHINA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI MKOA WA MWANZA, MAXIMILIAN NGEDERE @ TULA MIAKA 40, MKAZI WA MTAA WA KANYERERE, ALIMJERUHI KWA KUMPIGA RISASI KWA KUTUMIA BASTOLA YENYE BJ 306666 YENYE CAR NAMBA 00103129 MKEWE AITWAYE TEDY PATRICK MIAKA 38, MKAZI WA KANYERERE, SEHEMU YA MGONGONI NA KUTOKEZEA TUMBONI NA KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA KISHA AKAJIPIGA NA YEYE MWENYEWE RISASI YA KIFUANI MKONO WA KUSHOTO HALI ILIYOPELEKEA YEYE MWENYEWE KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO HUKU MKEWE AKIJERUHIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KUPATIWA MATIBABU AKIWA NA HALI MBAYA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

INASEMEKANA KUWA WAWILI HAO WALIKUWA WAFANYABIASHARA WA SAMAKI NA MWANAMUME ALIKUWA ANAMILIKI SILAHA TAJWA HAPO JUU KISHERIA, INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU WALIKUWA WAMERUDI KUTOKA KWENYE BIASHARA ZAO. INADAIWA KUWA PINDI WALIPOKUWA NDANI CHUMBANI WALISIKIKA WAKIWA WANAGOMBANA, NDIPO BAADA YA MUDA MCHACHE KUPITA ILISIKIKA MILIO YA RISASI KUTOKA CHUMBANI.
WATU/MAJIRANI WALIINGIA NDANI KUWASAIDIA NDIPO WALIMKUTA BI TEDY PATRICK AKIPIGA YOWE AKIWA AMEJERUHIWA KWA RISASI SEHEMU TAJWA HAPO JUU AKIOMBA MSAADA, HUKU MUMEWE AKIWA TAYARI AMEFARIKI DUNIA KWA KUJIPIGA RISASI, WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFIKA KWA HARAKA ENEO LA TUKIO NA KUMCHUKUA MAJERUHI BI TEDY PATRICK KISHA KUMKIMBIZA  HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KUPATIWA MATIBABU LAKINI LEO TAREHE 26.05.2017 MAJIRA YA SAA 09:30HRS ASUBUHI MAJERUHI ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KINACHUNGUZWA, POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO NA WENZI WAO AU WATU WENGINE, BALI WATOE TAARIFA KWA WAZEE WENYE BUSARA ILI WAWEZE KUSULUHISHA MIGOGORO HIYO KWA AMANI AU KWENYE VYOMBO VYA DOLA ILI KUEPUSHA VIFO NA MAJERUHI VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments