Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU MATUMIZI YA FOMU NAMBA 3 YA POLISI


watu
Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi kuwa, Fomu ya Polisi namba 3 ijulikanayo kama PF.3 hutolewa  kwa mtu baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji au muathirika  kwa matukio yenye madhara mwilini, ajali au  matukio yenye kuleta mashaka kuhusu vyanzo vyake kama vile kipigo, kujeruhi, ubakaji, kulawiti,  kunywa sumu na mengineyo.

Ieleweke wazi kwamba matumizi ya PF3 ni ya lazima na yanaendelea kama kawaida  kwa mujibu wa sheria, fomu hiyo inapaswa kutumika kwa kila tukio la aina tajwa hapo juu ili muathirika  aweze kupata matibabu katika vituo vya Afya na hatua za kiupelelezi  kwa Jeshi la Polisi ziweze kuendelea. 
Katika mazingira mengine hali ya muathirika inaweza kuwa mbaya, hivyo,  huduma za kuokoa maisha (huduma ya kwanza) zinaweza kuendelea kutolewa wakati watoa  huduma ya afya wakiijulisha Polisi  ili kuharakisha upatikanaji wa PF 3.
Imetolewa na:-
Advera Bulimba-ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

No comments