Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


msangii-1
TAREHE 15.05.2017 MAJIRA YA SAA 20:00HRS KATIKA KIJIJI CHA IBAYA KATA YA RUNELE TARAFA YA NYAMILAMA WILAYA YA KWIMBA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MEJA NTENDE MIAKA 35, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA IBAYA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA MUMEWE AITWAYE MBIMBE NYANDA MIAKA 45, FIMBO KICHWANI SEHEMU YA JUU YA JICHO LA KULIA WAKATI WAKIWA KWENYE UGOMVI NA KUPELEKEA MUMEWE KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO.

INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUA KWENYE UGOMVI NA MKEWE BI MEJA NTENDE, HII NI KUTOKANA NA KUUZA CHOROKO KIASI CHA KILO TATU ZENYE THAMANI YA TSH 2,400/= , BILA YA KUPEWA RUHUSA NA MUMEWE, LAKINI PIA PINDI ALIPOKWENDA SHAMBA ALIACHA JEMBE SHAMBANI. INASEMEKANA KUWA MAREHEMU ALICHUKIZWA NA VITENDO HIVYO HAPO JUU NDIPO ALIANZA KUMPIGA MKEWE KWA KUTUMIA NGUMI NA MATAKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE, HUKU AKIMLAZIMISHA KWAMBA LAZIMA ARUDISHE CHOROKO ALIZOZIUZA LAKINI PIA AENDE SHAMBANI KULETA JEMBE ALILOLIACHA.
AIDHA INADAIWA KUWA KATIKA HARAKATI ZA MWANAMKE KUJIOKOA KUTOKA KWENYE KIPIGO CHA MUMEWE ALIOKOTA FIMBO KISHA AKAMPIGA NAYO MAREHEMU KICHWANI SEHEMU YA JUU YA JICHO NDIPO MAREHEMU ALIANGUKA CHINI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO. WATU MAJIRANI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO. MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHANA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI WANANDOA AKIWATAKA PINDI WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO WAENDE KWA WAZEE AU VIONGOZI WAO WA MITAA AU VIJIJI ILI WAWEZE KUPATA SULUHISHO LA MATATIZO YAO NA SIO KUTUMIA VIPIGO KWANI NI UKATILI NA NI KOSA LA JINAI, LAKINI PIA VINAWEZA KULETA MADHARA MAKUBWA YA AINA KAMA HII YA MTU KUPOTEZA MAISHA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments