Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

indexTAREHE 08:05.2017 MAJIRA YA SAA 17:20HRS KATIKA BARABARA YA KIGONGOFERY – USAGARA KIJIJI CHA IDETEMYA TARAFA YA USAGARA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, MTU ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHARLES RENATUS MIAKA 55, MKAZI WA MKOLANI – MWANZA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA AJALI AKIWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA MC 570 BEE  ALIYOKUWA AKIENDESHA AKITOKEA KIGONGOFERY KWENDA MWANZA KUGONGANA NA PIKIPIKI NYINGINE YENYE NAMBA MC 222BFS AINA YA SUNLG ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MTU AITWAYE KURWA YANGA MIAKA 21, MKULIMA NA MKAZI WA ISAMILO ALIYEKUWA AKITOKEA USAGARA KWENDA KIGONGOFERY. NA KUMSABABISHIA MAJERAHA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE YEYE PAMOJA NA ABIRIA ALIYOKUWA AMEBEBWA NA MAREHEMU  AITWAYE SEMENI SHIJA MIAKA 21 MKAZI WA ISAMILO.

CHANZO CHA AJILI NI MWENDO KASI KWA MADEREVA WOTE WAWILI HALI  ILIYOPELEKEA KUISHINDWA KUMUDU PIKIPIKI ZAO NA KUSABABISHA AJALI KUTOKEA, MBAYA ZAIDI MADEREVA WOTE WALIKUWA HAWAJAVAA KOFIA NGUMU. MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALI YA BUKUMBI KWA AJILI YA MATIBABU  LAKINI HALI ZAO BADO SIO NZURI, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO HUSUSANI PIKIPIKI  AKIWATAKA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI PINDI WAWAPO BARABARANI ILI KUEPUSHA VIFO NA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA:
DCP; AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments