Header Ads

Responsive Ads Here

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UGENI KUTOKA UDART LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TELEGRAMS:   POLISI,                                                                                               OFISI YA
TELEPHONE: 2500712                                                                         KAMANDA WA POLISI,
Fax: 2502310                                                                                            MKOA WA MWANZA,
E-mail: mwapol@yahoo.com                                                                                      S.L.P. 120,
           rpc.mwanza@tpf.go.tz                                                                                  MWANZA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 30.05.2017.
  • MUME AFARIKI DUNIA NA MWANAMKE KUJERUHIWA VIBAYA BAADA YA WAO WENYEWE KUPIGANA KWA KUTUMIA VITU VYENYE NCHA KALI WILAYANI UKEREWE.
  • MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI MISOKOTO 30 WILAYANI ILEMELA.
  • MWANAMKE MMOJA AMEKUTWA AKIWA AMEFARIKI DUNIA CHUMBANI KWAKE HUKU MWILI WAKE UKIWA NA MAJERAHA BAADA YA KUPIGWA NA MUMEWE WILAYANI ILEME
KATIKA TUKIO LA KWANZA;
KWAMBA TAREHE 29.05.2017 MAJIRA YA SAA 10:15HRS ASUBUHI KATIKA KITONGOJI CHA KAMENGO KIJIJI CHA MURITI TARAFA YA ILANGALA WILAYA YA UKEREWE MKOA WA MWANZA, MWANAMUME MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MELKIAD MISANA MIAKA 50, MKULIMA NA MKAZI WA MIRITI, AMEFARIKI DUNIA WAKATI AKIKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI MGONGONI UPANDE WA KUSHOTO NA MKEWE, HUKU MKEWE AITWAYE BUKHEHERE WILLIUM MIAKA 25, AKIJERUHIWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KWENYE MIKONO YOTE MIWILI , MATITI NA TUMBONI AMBAPO UTUMBO ULITOKA NJE NA MAREHEMU MUMEWE BAADA YA KUZUKA KWA UGOMVI KATI YAO KISHA KUCHOMANA NA VITU VYENYE NCHA KALI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA USIKU WA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAREHEMU HAKULALA NYUMBANI KWAKE LAKINI ALIRUDI NYUMBANI ASUBUHI AKIWA AMELEWA KITENDO AMBACHO HAKIKUMFURAHISHA MKEWE BI BUKHEHERE WILLIUM. KUTOKANA NA HALI HIYO WAWILI HAO WALIJIKUTA WAKIINGIA KWENYE UGOMVI KISHA KUANZA KUPIGANA KWA KUTUMIA VITU VYENYE NCHA KALI KWA KILA MMOJA KUMCHOMA MWENZAKE KWENYE MAENEO TAJWA HAPO JUU, HALI ILIYOPELEKEA KILA MMOJA BAADA YA MUDA MCHACHE KUPITA  KUPOTEZA FAHAMU.
INASEMEKANA KUWA BAADA MAJIRANI KUSIKIA VURUGU HIZO WALIKWENDA ENEO LA TUKIO KUTOA MSAADA KISHA WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA KUHUSIANA NA TAARIFA HIZO AMBAPO WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUWAKIMBIZA MAJERUHI HOSPITALI, NDIPO WAKATI WAKIWA NJIANI MWANAMUME ALIPOTEZA MAISHA HUKU MKEWE AKIWA KATIKA HALI MBAYA HAJITAMBUI.
MAJERUHI BI BUKHEHERE WILLIUM AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA UKEREWE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU LAKINI HALI YAKE BADO SIO NZURI HUKU AKIWA CHINI YA ULINZI WA ASKARI POLISI. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI KUHUSIANA NA MAUJI HAYO, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO KWA AJILI YA UCHUNGUZI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI WANANDOA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO NDANI YA FAMILIA KWANI NI KOSA KISHERIA, BALI WAPELEKE MATATIZO YAO KWA WAZEE, VIONGOZI WA MITAA AU KWENYE VYOMBO VYA DOLA ILI KUEPUSHA MAJERAHA NA VIFO VYA AINA KAMA HII VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI,
MNAMO TAREHE 29.05.2017 MAJIRA YA SAA 16:45HRS KATIKA MTAA WA NYAMHONGOLO KATA YA NYAMHONGOLO WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MWANAMKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SUZANA WISTON MIAKA 18, MKULIMA NA MKAZI WA NYAMHONGOLO AKIWA NA MISOKOTO 30 YA BHANGI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI ASKARI WAKIWA  DORIA WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA WASIRI KWAMBA MAENEO TAJWA HAPO JUU WAPO WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI, ASKARI WALIFANYA UPELELEZI NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TAARIFA HIZO
NDIPO MAJIRA TAJWA HAPO JUU WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA HUKU AKIWA NA MISOKOTO 30 YA BHANGI.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HIYO HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI VIJANA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA UTUMIAJI, USAFIRISHAJI NA UUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA KWANI YATAWAIINGIZA KWENYE MATATIZO BALI WAFANYE KAZI HALALI ZA KUWAPATIA KIPATO.
KATIKA TUKIO LA TATU,
KWAMBA TAREHE 30.05.2017 MAJIRA YA SAA 03:09HRS ALFAJIRI KATIKA MAENEO YA MTAA WA PASIANSI MASHARIKI KATA YA PASIANSI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ESTER CHARLES MIAKA 30, MAKAZI WA PASIANSI MASHARIKI AMEKUTWA AKIWA AMEFARIKI DUNIA CHUMBANI KWAKE ALIPOKUWA AKIISHI NA MUMEWE AITWAYE CHARLES JOHN MIAKA 35, HUKU MWILI WAKE UKIWA NA MAJERAHA SEHEMU MBALIMBALI YA MWILI WAKE, HII BAADA YA KUZUKA KWA UGOMVI KATI YAO KISHA KUPIGWA NA MUMEWE NA BAADAE MWANAMUME KUTOROKA KUSIKO JULIKANA.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI HAPO NYUMBANI KWAO NA MUMEWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHARLES JOHN MKAZI WA PASIANSI MASHARIKI, LAKINI KWA KIPINDI CHOTE WAKIWA KWENYE MAHUSIANO  WAWILI HAO WALIKUWA KWENYE MIGOGORO YA MARA KWA MARA YA NDANI YA FAMILIA KWANI MWANAMKE ALIKUWA AKIMTUHUMU MUMEWAKE KWAMBA ANATOKA NJE YA NDOA.
INASEMEKANA KUWA TAREHE TAJWA HAPO JUU USIKU MAJIRANI WALISIKIA UGOMVI UKIENDELEA KATI YA WAWILI HAO HUKU MWANAMKE AKIPIGA KELELE AKIOMBA MSAADA, LAKINI MAJIRANI HAWAKWENDA KUWASAIDIA KWANI WALIZOEA KUWASIKIA WAKIPIGANA NA BAADAE KUELEWANA KISHA KUENDELEA NA MAISHA KAMA KAWAIDA.
INADAIWA KWAMBA BAADA YA MUDA KUPITA HAPAKUSIKIKA TENA UGOMVI HIVYO MAJIRANI WALIJUA TAYARI WAMEELEWANA, LAKINI BAADAE ALISIKIKA MTOTO AKILIA KWA MUDA MREFU NDIPO MAJIRANI WALIKWENDA DIRISHANI KUANGALIA NA KUMUONA MAMA YAKE AKIWA AMELALA KIMYAA KITANDANI BILA KUMSAIDIA MTOTO HUKU BABA YAKE AKIWA HAYUPO, BAADA YA KUONA HALI HIYO MAJIRANI WALIPATA MASHAKA KISHA WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI.
POLISI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA KUSIANA NA TAARIFA HIYO HADI ENEO LA TUKIO KISHA KUMKUTA MWANAMKE TAJWA HAPO JUU AKIWA TAYARI AMEPOTEZA MAISHA, HUKU MWILI WAKE UKIWA NA MAJERAHA YA KUPIGWA NA KITU KIZITO MAENEO MBALIMBALI YA MWILI WAKE NA SHINGONI KWAKE KUKIONEKANA KUKABWA NA KITAMBAA KIGUMU NA MUMEWE ALIYEKUWA WAKIPIGANA KISHA BAADA YA KUONA MKEWE AMEFARIKI DUNIA ALITOROKA KUSIKO JULIKANA.
POLISI WAPO KWENYE MSAKO MKALI WA KUHAKIKISHA MTUHUMIWA WA MAUJI HAYO ANAKAMTWA, AIDHA PIA UPELELEZI KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO BADO UNAENDELEA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHI HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYA ILI AWEZE KUKAMATWA HARAKA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE WENYE TABIA ZA AINA KAMA HII, LAKINI PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA KISHERIA NA PIA INAWEZA KUSABABISHA MATATIZO YA AINA KAMA HII AMBAYO YANAWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments