Header Ads

Responsive Ads Here

SMZ KUIMARISHA MASHIRIKIANO NA JUMUIYA ZA KIKANDA


usi ha
Na Ali Issa- Maelezo Zanzibar 15/05/2015
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuimarisha mashirkiano na Jumuiya za Kikanda na Kimataifa na kuwashirikisha ipasavyo Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi  ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu wakati alipokuwa akiwasilisha Hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/2018 huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
 Amesema mafanikio hayo yatapatikana kupitia utekelezaji wa Programu hiyo ambapo Zanzibar itafaidika na fursa za kiuchumi na Kijamii zinazotokana na Jumuiya za Kikanda na kimatifa na Wazanzibari wanoishi nje ya Nchi.
Waziri Gavu amesema ili kufikia malengo ya Programu hiyo shughuli mbalimbali zimepangwa kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa Mtangamano wa jumuiya za kikanda na dhana ya Diaspora na umuhimu wake kwa maendeleo ya jamii.
Shughuli nyingine ni utekelezaji wa Mpango kazi wa Sera ya Diaspora na kuandaa Kongamano la Watanzania wanaoishi nje ya nchi.  
Mbali na shughuli hizo Wizara hiyo pia imejipanga kutekeleza Vipaumbele vyake ambavyo ni pamoja na kuendeleza ujenzi na kuimarisha usalama wa nyumba za Ikulu.
Sambamba na hayo Wizara hiyo pia itaendelea kuwahudumia Wananchi kwa kuzitekeleza ahadi za Rais wa Zanzibar pamoja na kuwapatia taarifa za shughuli za Serikali na maendeleo ambayo ni haki ya kikatiba.
Waziri Gavu amesema ili kufikia malengo yaliyokusudiwa analiomba Baraza limuidhinishie makadirio ya matumizi ya programu za ofisi ya Rais na Menyekiti wa baraza la mapinduzi jumla Tzs 8,342.6 milioni. Kati ya fedha hizo Tzs 7,612.6 milioni kwa ajili ya matumizi ya kazi za kawaida na Tzs 730.0 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya mendeleo.  

No comments