Header Ads

Responsive Ads Here

SIMBA YAREJEA KIMATAIFA,YAIBUTUA MBAO FC


Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa taji ls Azam Sports Federation Cup (FA Cup) baada ya kuifunga Mbao bao 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ushindi wa Simba umewapa ubingwa wa kombe, pesa kiasi cha shilingi milioni 50 za Tanzania pamoja na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Ilikua ni fainali ya aina yake, soka likapigwa kwa kiwango cha juu na kuburudisha mashabiki walioujaza uwanja wa Jamhuri kushuhudia fainali iliyozikutanisha timu mbili, moja ikitoka Magharibi mwa Tanzania huku nyingine maskani yake yakiwa ni Mashariki.
Dakika 90 zilimalizika timu zote zikiwa hazijafungana na kulazimika kuongezwa dakika 30 za kuendelea kumtafuta bingwa mwa mwaka 2017.
Simba walipata bao lao la kwanza dakika 15 za kwanza za muda wa nyongeza kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Ivory Coast Fredrick  Blagnon.
Mbao walipambana na kusawazisha bao hilo kipindi cha pili cha dakika za nyongeza na kuwaongezea Simba mlima ambapo baadhi ya mashabiki walitumaini mchezo ungemalizika kwa Simba kushinda 1-0.
Kipenzi cha wanamsimbazi Shiza Kichuya akaipa Simba ndoo kwa kuifungia goli kwa mkwaju wa penati kufuatia beki wa Mbao kuushika mpira akiwa kwenye eneo la hatari wakati akifanya harakati za kuokoa.
IMG_0015
Penati hiyo ilizua utata baada ya wachezaji wa Mbao kuanza kumzonga mwamuzi wakipinga maamuzi yake hadi askari polisi wakalazimika kuwatuliza wachezaji wa Mbao na kuweka mwamuzi katika hali ya usalama.

No comments