Header Ads

Responsive Ads Here

SIMBA YAKIMBILIA FIFA KISA MCHEZAJI WA KAGERA SUGAR


aveva2
Klabu ya Simba imesema kuwa, itapeleka malalamiko yao katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutokana na kudhulumiwa mchezaji wao, Mbaraka Yusuph anayekipiga kwenye kikosi cha Kagera Sugar.
 
Rais wa Simba, Evans Aveva, ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari huku akiwa na leseni mkononi ya mchezaji huyo inayoonesha mwanzoni mwa msimu huu walimsajili ili aitumikie Simba, lakini wakashangaa anaichezea Kagera Sugar.
 
“Mbaraka Yusuph jina lake pamoja na majina yote ya wachezaji wetu wa msimu huu tuliyawasilisha TFF na tukapewa leseni zao wote kuidhinisha kwamba tuwatumie msimu huu. Cha kushangaza tukaona anaichezea Kagera Sugar.
 
“Malalamiko yetu yapo TFF kwa muda mrefu lakini mpaka sasa hatujapewa majibu yoyote, sasa tunaamua kwenda Fifa kudai haki yetu juu ya mchezaji huyu ambaye leseni yake inayoonyesha ni mchezaji wetu tunayo mpaka sasa,” alisema Aveva.

No comments