Header Ads

Responsive Ads Here

SERIKALI YAWAPONGEZA WANANCHI WALIONDOA MAKAZI YAO KATIKA HIFADHI KWA HIARI.


ramo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto) akikagua maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Isawima Wilayani Kaliua hivi karibuni.

Na Tiganya Vincent-Kaliua
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amewashukuru wavamizi  wa Msitu wa Hifadhi wa Isawima wilayani Kaliua ambao wameamua kwa hiari yao kubomoa makazi na kuondoka wao na mifugo yao katika eneo hilo ambalo ni miongoni mwa vyanzo vya maji ya Ziwa Tanganyika .
Prof. Maghembe alitoa kauli hiyo jana Wilayani Kaliua baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa Wavamizi wa Msitu huo wa Hifadhi, na kutembelea eneo walipoondolewa wavamizi na kisha kupata fursa ya kuongeza na wananchi.
Alisema kuwa Serikali imefurahishwa na uamuzi huo uliochukuliwa na watu hao baada ya kupata elimu kuhusu athari za kimazingira za wao kung’ang’ania kuendelea kuishi katika maeneo yaliyohifadhiwa na kuamua kuondoka bila kushurutishwa.
Prof. Maghembe aliongeza kuwa Serikali haina shida ya kumuonea  mtu na ndio maana imekuwa ikutumia zaidi elimu jambo ambalo limeleta mafaniko makubwa katika eneo la Hifadhi hiyo ambapo zaidi ya asilimia ya 70 ya watu waliokuwa wamevamia waliondoka na kuishi katika makazi wengi ya watu.
Alisisitiza kwa wale waliokaidi kuondoka katika Mistu ya Hifadhi kwa hiari ni wale wanaoendesha vitendo vya uharifu kama vile uwindaji haramu wa wanyama wakiwemo tembo na kilimo cha bangi.
Prof. Maghembe alisema kuwa Serikali iko makini itapambana na wale wote wanaokaidi kuondoka katika maeneo ya hifadhi kwa lengo la kuhujumu rasimali za Taifa na kulima mazao kama vile bangi.
Aidha , Waziri huyo aliipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kaliua na Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya Isawima kwa jinsi walivyoendesha zoezi hilo kirafiki na kuhakikisha wavamizi wanaondoka na kubomoa wenyewe kwa hiari majengo yalikuwemo katika eneo la hifadhi hiyo.
Alitoa wito kwa wananchi waliondoka katika Hifadhi hizo na wanaishi jirani ya hapo wawe  walinzi wa mipaka ya hifadhi na kuhakikisha kuwa hakuna mtu yoyote atakayeingia katika hifadhi hiyo.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wavamizi wa Misitu ya Mpandaline na North Ugalla ,Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw.Abel Busalama alisema kuwa elimu ilisaidia watu kutikia kwa wingi zoezi la kuwaondoa katika maeneo ya hifadhi na kuanza wao wenyewe kubomoa nyumba na kuchukua kile walichoona kitawafaa.
Bw.Busalama alimweleza Waziri huyo kuwa wavamizi wengi wao walikuwa wakiendesha shughuli zao mpaka kwenye shoroba(njia za wanyama) na kuwafanya kuhamia nyingine kwa hofu ya usalama wao.
Aliongeza wengine walikuwa wanaendesha shughuli za kilimo na ufugaji kiasi cha kuharibu mistu na kusababisha maji yanakwenda Mto Malagarasi  kupungua na hivyo kuathiri Ziwa Tanganyika.
Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa katika kutekeleza zoezi hilo walifanikiwa kukamata ng’ombe 10121, mbuzi 60 na kondoo 22 na kukusanya  jumla ya shilingi milioni 409 zimkusanywa.

No comments